VIPOPOO VYA MCHELE

Vipopoo vya Kiasili vya Unga wa Mchele 🥥✨ 📝 Mahitaji: Mchele – 2 vikombe Maji – vya kutosha kwa kurowekea na kupikia Uwanga (Corn flour/Starch) – kiasi cha kushikilia viduara Tui jepesi la nazi – 2 vikombe Tui zito la nazi – 1 kikombe Sukari – ½ kikombe (au kulingana na ladha) Hiliki ya unga – 1 kijiko cha chai Zabibu kavu – kwa kupambia 👨🍳 Namna ya Kutayarisha: 🔹 Hatua ya 1: Kuandaa Unga wa Mchele 1️⃣ Roweka mchele kwa masaa 2 ili kulainika. 2️⃣ Chuja maji kisha kausha mchele juani hadi uwe mkavu. 3️⃣ Saga mchele kupata unga laini. 🔹 Hatua ya 2: Kutengeneza Vipopoo 4️⃣ Songa unga huu kama ugali , hadi uwe laini. 5️⃣ Tengeneza viduara vidogo, ukitumia uwanga ili visishikane. 6️⃣ Weka viduara hivyo juani hadi vikauke kabisa. 🔹 Hatua ya 3: Kupika Vipopoo 7️⃣ Chemsha maji kwenye sufuria, kisha tia vipopoo na uvipike hadi viive na vilainike. 8️⃣ Chuja maji na weka vipopoo pembeni. 🔹 Hatua ya 4: Kutayarisha Mchuzi 9️⃣ Chemsha tui jepesi ...