MAKARONI YA NYAMA YA KUSAGA
JINSI YA KUPIKA MAKARONI YA NYAMA YA KUSAGA
VIPIMO:
- 🍝 Makaroni - 500 gm
- 🥩 Nyama ya kusaga - 450 gm
- 🧅 Vitunguu - 2
- 🍅 Nyanya - 3
- 🍅 Nyanya kopo (Tomato Paste) - Vijiko vya supu 3
- 🧄 Kitunguu thomu (Garlic), kilosagwa - Kijiko cha chai 1
- 🌶️ Pilipili manga - Kijiko cha chai 1
- 🌿 Bizari ya oregano [Italian spice] - Kijiko cha chai 1
- 🌱 Parsely (aina ya kotmiri) - Misongo (bunches) 2
- 🍶 Sosi ya soya - Vijiko vya supu 2
- 🛢️ Mafuta - Kikombe cha chai ¼
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA:
1️⃣ Chemsha makaroni kama inavyoelekezwa kwenye paketi hadi yaive lakini yasivurugike. Chuja maji na weka kando.
2️⃣ Katakata vitunguu na nyanya vipande vidogo vidogo kisha weka kando.
3️⃣ Katakata parsley ndogo ndogo (chopped) kisha weka kando.
4️⃣ Weka mafuta kwenye sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kidogo.
5️⃣ Ongeza nyama ya kusaga, kitunguu thomu, na bizari zote. Endelea kukaanga hadi nyama iwive.
6️⃣ Ongeza nyanya, nyanya kopo, parsley, na sosi ya soya. Endelea kukaanga kwa muda mfupi tu.
7️⃣ Ongeza makaroni kwenye mchanganyiko huo na changanya vizuri.
8️⃣ Pakuwa kwenye bakuli au sahani na ikishakuwa tayari kwa kula.
😋 Furahia makaroni ya nyama ya kusaga!
Maoni