🥮🌺VILEJA VYA TAMBI
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
JINSI YA KUPIKA VILEJA VYA TAMBI
VIPIMO
🍝 Tambi (vermicelli Roasted): Mifuko 2
🧈 Siagi: 4 vijiko vya supu
🥛 Maziwa (condensed): 300ml
🥜 Lozi zilizokatwakatwa: 1 kikombe
🍇 Zabibu kavu: 1 kikombe
🌸 Arki (essence): 1 kijiko cha supu
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1️⃣ Weka karai kwenye moto kiasi.
2️⃣ Tia 🧈 siagi na uache iyeyuke.
3️⃣ Tia 🍝 tambi, uzikaange bila kuacha mkono hadi ziwe na rangi ya dhahabu.
4️⃣ Ongeza 🥜 lozi na 🍇 zabibu, huku ukiendelea kukoroga.
5️⃣ Mimina 🥛 maziwa na endelea kukoroga bila kuacha mkono.
6️⃣ Tia 🌸 arki, na koroga ili ichanganyike vizuri.
7️⃣ Epua karai na tumia kijiko cha chai kuchota mchanganyiko, kisha uweke kwenye kikombe cha kahawa nusu (usikijaze).
8️⃣ Kipindue kwenye sahani ili kutoa kileja.
9️⃣ Rudia hatua hii mpaka umalize mchanganyiko wote.
Furahia vileja vyako vitamu vya tambi! 🥰
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni