π₯JINSI YA KUPIKA MEATROLL TAMU
π MAHITAJI
✅ 1 kikombe siagi π§
✅ 2 vikombe unga wa ngano πΎ
✅ Maji kiasi π§
✅ 1 kikombe nyama ya kusaga π₯©
✅ ½ kijiko cha chai pilipili manga ya unga πΆ️
✅ ½ kijiko cha chai kitunguu saumu (thomu) iliyosagwa π§
✅ ½ kijiko cha chai tangawizi iliyosagwa π±
✅ Chumvi kiasi π§
π JINSI YA KUTAYARISHA
1️⃣ Pika nyama – Changanya nyama, pilipili manga, thomu, tangawizi na chumvi ndani ya sufuria.
Pika bila mafuta wala maji, huku unaikoroga koroga hadi iwe kavu.
Epua na weka pembeni.
2️⃣ Tengeneza unga – Changanya unga na siagi hadi uchanganyike vizuri.
Ongeza maji kiasi ili ushikane, lakini usiukande sana.
3️⃣ Sukuma na kata – Kata madonge na usukume kama unavyotengeneza chapati, lakini usiufanye mwembamba sana.
Kata vipande virefu (rectangular).
4️⃣ Funga nyama – Weka nyama juu ya kila kipande cha unga.
Kunja upande mmoja kufunika nyama.
Kunja upande wa pili kufunika sehemu ya kwanza.
5️⃣ Tengeneza nakshi – Tumia uma kuchoma choma juu ya meat roll ili kuweka muonekano mzuri.
Hii pia inadidimiza sehemu ya mwisho ili isifunuke wakati wa kuoka.
6️⃣ Oka – Paka siagi kwenye tray kisha panga meat rolls zako.
Washa oven kwa 350°C na osha hadi zibadilike rangi kuwa za dhahabu.
7️⃣ Ziko tayari! – Zilaze kidogo zipowe, kisha zifurahie kwa chai, supu au kama kitafunwa cha mchana! π₯π
π₯ VIDOKEZO VYA MAFANIKIO
✔️ Usikande unga sana ili meat rolls ziwe laini na si ngumu.
✔️ Usipike nyama na mafuta – inapaswa kuwa kavu ili isiwarike unga wakati wa kuoka.
✔️ Oka hadi ziwe za kahawia dhahabu ili ziwe na ladha bora.
✔️ Unaweza kuzipaka yai juu kabla ya kuoka kwa muonekano mzuri.
π₯ Furahia Meat Roll zako zenye ladha tamu! π₯©π₯
Maoni