🌿🥩🍌NDIZI ZA NYAMA
NAMNA YA KUPIKA NDIZI ZA NYAMA
MAHITAJI
🍌 Ndizi mbichi - 10-12
🥩 Nyama ng’ombe - 1 kilo moja
🧅 Kitunguu maji - 2
🍅 Nyanya/tungule - 2
🧄 Kitunguu saumu (thomu/galic) - 7
🧑🍳 Tangawizi mbichi - 1 kipande
🍋 Ndimu - 2 kamua
🧂 Chumvi - kiasi
🛢 Mafuta - 3 vijiko vya supu
🥥 Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- 🧄 Saga kitunguu thomu na tangawizi mbichi.
- 🥩 Weka nyama katika sufuria, tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi, na ndimu, kisha chemsha hadi iive.
- 🍌 Menya ndizi na ukatekate.
- 🛢 Weka mafuta katika sufuria, tia kitunguu maji kilokatwakatwa, ukaange kidogo tu, kisha tia nyanya/tungule uendelee kukaanga.
- 🧄 Tia tangawizi na thomu iliyobakia.
- 🍌 Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake.
- 🍽 Ziache ndizi ziive, zikiwa tayari tia tui la nazi.
Maoni