🍪🍯VILEJA VYA CARAMEL
JINSI YA KUPIKA VILEJA VYA CARAMEL🍪🍯
HATUA ZA MATAYARISHO
1️⃣ Saga siagi yako 🧈 kwenye bakuli hadi iwe laini.
2️⃣ Ongeza icing sugar 🍬 100g na uendelee kusaga hadi mchanganyiko uwe laini na ulainike vizuri.
3️⃣ Weka yai 🥚 1 na uchanganye hadi litachanganyika vizuri kabisa.
4️⃣ Ongeza arki 🌸 unayopenda kwa ladha, koroga kidogo tena, kisha zima mashine ya kusagia.
5️⃣ Weka nusu ya kijiko kimoja cha baking powder 🧂, kijiko 1 cha chakula cha caramel sauce 🍯, na chumvi 🧂 kidogo sana (robo kijiko cha chai). Koroga taratibu kwa kutumia mwiko mpaka vichanganyike vizuri.
6️⃣ Ongeza unga wa ngano 🌾 kidogo kidogo huku ukichanganya kwa mkono mpaka upate donge lisilonyata. Ukande donge kwa dakika 1.
7️⃣ Gawa donge mara mbili sawa.
8️⃣ Chukua kipande kimoja, uviringishe kuwa duara, kisha usukume kama chapati (lisiwe nene sana).
9️⃣ Tumia kibati chenye kishimo kisichopenya upande wa pili kukata shapes na kutengeneza shimo katikati kwa ajili ya caramel.
🔟 Rudia hatua hiyo kwa donge lote.
1️⃣1️⃣ Panga vileja vyako kwenye trey ya kuchomea.
1️⃣2️⃣ Choma kwa moto wa 180°C/350°F kwa dakika 10-15.
1️⃣3️⃣ Vileja vikishaiva, vitoe kwenye oven na uviache vipowe.
1️⃣4️⃣ Jazia caramel sauce 🍯 kwenye vile vishimo.
1️⃣5️⃣ Pamba kwa vipipi 🌟 kama unataka.
Furahia vileja vyako vya caramel! 🍪🍯
Maoni