- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
NAMNA YA KUPIKA BIRIANI YA NYAMA YA NG'OMBE
VIPIMO VYA MASALA
- Nyama vipande: 3 LB π₯©
- Mtindi: ½ kopo π₯
- Kitunguu (thomu/galic): 1½ kijiko cha supu π§
- Tangawizi: 1½ kijiko cha supu πΏ
- Nyanya: 2 π
- Pilipili mbichi: kiasi πΆ️
- Nyanya kopo: 4 vijiko vya supu π
- Vidonge supu: 2 π
- Pilipili nyekundu paprika: kiasi πΆ️
- Bizari zote saga: 2 vijiko vya supu πΏ
- Viazi: 4 π₯
- Mafuta: 2 mug π’️
- Samli: ½ kikombe π§
- Vitungu: 6 π§
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Kwenye sufuria, tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, na tangawizi.
- Mimina kwenye nyama na mtindi, tia nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi, kisha changanya vyote pamoja na weka motoni.
- Katika sufuria nyingine, tia mafuta na samli, kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi, kisha toa na weka pembeni.
- Kanga viazi na weka pembeni.
- Chukua mafuta kidogo uliyokangia, tia kwenye nyama, acha kwenye moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke.
- Tia viazi na vitunguu vivunje-vunje, tia ndani ya nyama, acha moto mdogo.
Vipimo Vya Wali π
- Mchele - 5 mug π
- Maji - kiasi π§
- Chumvi - kiasi π§
- Mafuta uliyokaanga vitungu - kiasi π§
- Rangi ya biriani - ¼ kijiko cha chai π
- Zafarani - ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutarisha Na Kupika Wali
- Osheni mchele na uroweke kwa saa. π§Όπ
- Chemsha maji, kama magi 10 hivi, na chumvi. π§π§
- Tia mchele kwenye maji na uache uchemke mpaka kiini kiive nusu. π
- Mwaga maji na chuja. ππ§
- Mimina mchele juu ya nyama, tia rangi na mafuta kwa juu, kisha funika. ππ
- Acha kidogo kwenye oveni kwa dakika 20 hivi, kisha epua ikiwa tayari. π₯⏲️
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni