BUNS/SCONES ZA SUKARI
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA BUNS/SCONES ZA SUKARI NYUMBANI
- 🥣 Unga - 3 vikombe vya chai
- 🥛 Maziwa - 1 kikombe cha chai
- 🍚 Sukari - ¼ kikombe cha chai
- 🧈 Siagi - ¼ kikombe cha chai
- 🧂 Chumvi - ½ kijiko cha supu
- 🍳 Yai - 1
- 🍞 Hamira - 2 ¼ vijiko vya chai (pakiti 1)
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA:
1️⃣ Changanya sukari na ½ kikombe cha maziwa yaliyo vuguvugu kwenye kibakuli, kisha tia hamira, koroga vizuri na wachia kwa dakika 5.
2️⃣ Tia yai, yale maziwa yaliyobakia (½ kikombe) na siagi iliyoyeyushwa.
3️⃣ Katika bakuli nyingine, changanya unga na chumvi, kisha ongeza mchanganyiko wa hamira.
4️⃣ Kande unga vizuri baada ya kuinyunyizia unga kidogo ili isishike.
5️⃣ Laza unga katika friji kwa dakika kadhaa kwa ladha bora, kisha kata viduara 16 na vieke kwenye trei ya kuchomea iliyopakwa siagi.
6️⃣ Ziache katika sehemu yenye joto hadi zemuke.
7️⃣ Washa oveni kwa moto wa 350ºF.
8️⃣ Piga yai na kijiko kimoja cha maziwa, kisha paka juu ya buns kabla ya kuchoma.
9️⃣ Vumbika kwenye oveni kwa dakika 15 au hadi zibadilike rangi na kuwa zaidi ya za kupendeza!
Maoni