MKATE WA MCHELE/SINIA/KUMIMINA (Rice Cake)
MKATE WA MCHELE/SINIA/KUMIMINA (Rice Cake)
MAHITAJI:
- 🍚 Mchele - 2 vikombe (vip bora kwa mikate na vitumbua)
- 🍯 Hamira - 1 1/2 kijiko cha chai
- 🥥 Tui la nazi zito - 1 1/2 kikombe
- 🍬 Sukari - 1 kikombe
- 🌿 Hiriki ilopondwa - kiasi
- 🥚 Ute wa yai - 1 (ukipenda)
NAMNA YA KUPIKA:
1️⃣ Hatua ya 1:
- Loweka mchele katika maji kwa masaa kadhaa au usiku mzima ili ulainike.
2️⃣ Hatua ya 2:
- Chuja maji yote kisha tia mchele katika blender pamoja na tui la nazi na hiriki, saga hadi mchanganyiko usagike na kubaki na chenga chenga kidogo.
3️⃣ Hatua ya 3:
- Tia hamira na sukari kisha saga tena ili kuchanganya vizuri.
- Mimina mchanganyiko katika bakuli, funika na acha sehemu yenye joto ili ufure hadi ujazwe mara mbili.
4️⃣ Hatua ya 4:
- Ukiumuka, tia ute wa yai na sukari zaidi kama unahitaji, kisha koroga vizuri ili kuchanganya.
5️⃣ Hatua ya 5:
- Washa oven kwa joto la 180°C.
- Paka chombo chako mafuta kisha tia mchanganyiko katika sufuria jikoni juu ya moto wa wastani.
- Acha kwa muda wa dakika 1 kisha tia sufuria katika oven na oka kwa dakika 30-35 au hadi upate rangi nzuri juu na mkate uwe umeiva.
6️⃣ Hatua ya 6:
- Acha mkate upoe kabisa katika chombo chake kabla ya kuliwa.
🔥 Vile vya kupikia kwenye mkaa pia vinatoa ladha nzuri! Enjoy!
Maoni