🧆🔥 JINSI YA KUPIKA BAGIA ZA DENGU 🔥🧆
📌 Mahitaji:
🥣 Unga wa dengu – 3 vikombe vikubwa
🧂 Chumvi – 1 kijiko cha chai
💧 Maji baridi – 1 glasi
🌟 Baking powder – 1 kijiko cha chai
🌿 Majani ya kotmiri yaliyokatwakatwa – kiasi
🧅 Kitunguu maji kiliosagwa – 2 vijiko vya supu
🧄 Kitunguu saumu (thomu) kiliosagwa au unga – 1 kijiko cha chai
🛢️ Mafuta – kiasi cha kutosha kwa kukaanga
📝 Jinsi ya Kutayarisha na Kupika:
1️⃣ Kuandaa mchanganyiko
🔹 Katika bakuli lenye nafasi, mimina unga wa dengu na viungo vyote.
🔹 Tumia uma au kijiko kuvuruga mpaka upate mchanganyiko laini bila mabonge.
🔹 Hakikisha si mzito sana wala mwembamba sana.
🔹 Acha mchanganyiko upumzike kwa dakika 15-20 ⏳.
2️⃣ Kukaanga Bagia
🔥 Weka karai au sufuria nzito jikoni, mimina mafuta na acha yapate moto vizuri.
🥄 Tumia kijiko cha chakula kuchota mchanganyiko na mimina kwa uangalifu kwenye mafuta.
🔄 Geuza bagia upande wa pili hadi ziive na kupata rangi ya kahawia mpauko 🟤.
3️⃣ Kutoka jikoni
🥢 Tumia chombo chenye matundu (kama mwiko wa kukaangia) kutoa bagia na kuchuja mafuta yaliyobaki.
🍽️ Badilisha kwenye sahani na ziache zipowe kidogo.
😋 Zimeiva! Furahia bagia zako moto moto na chai au chutney! ☕🥣🔥

Maoni