🍗🍛BIRIANI YA KUKU WA KUCHOMA (GRILLED CHICKEN BIRIANI)
JINSI YA KUPIKA BIRIANI YA KUKU WA KUCHOMA (GRILLED CHICKEN BIRIANI)
MAHITAJI NA VIPIMO
🍚 Mchele wa Basmati/Pishori - 4 vikombe
🍗 Kuku
🧅 Vitunguu - 3
🍅 Nyanya/Tungule - 2
🫚 Tangawizi mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
🧄 Kitunguu saumu (thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
🌶️ Pilipili mbichi nzima - 3
🍋 Ndimu - 2
🍛 Garama Masala/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu
🌿 Haldi/tumeric/bizari manjano - 1 kijiko cha chai
🌶️ Pilipili ya unga nyekundu - 1 kijiko cha chai
🥛 Mtindi/Yoghurt - 3 vijiko vya supu
🛢️ Mafuta - ½ kikombe
HATUA ZA UPISHI
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- 🌀 Osha mchele, kisha roweka.
- 🧼 Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi na uweke katika bakuli.
- 🥣 Katika kibakuli kidogo, changanya:
- 🫚 Tangawizi mbichi
- 🧄 Thomu
- 🍛 Bizari zote
- 🌶️ Pilipili nyekundu ya unga
- 🧂 Chumvi
- 🥛 Mtindi
- 🍋 Ndimu (kamua).
- 🥄 Punguza mchanganyiko kidogo weka kando.
- Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku na uchanganye vizuri ili kuku arowanike (marinate) kwa dakika chache, hata nusu saa au zaidi.
- 🍗 Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni, kisha mchome (grill) huku ukiwa unageuzageuza hadi aive. Epua na weka kando.
- 🧅 Katakata vitunguu, 🍅 nyanya/tungule, na 🌶️ pilipili boga, kisha weka kando.
- 🛢️ Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta na kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
- Tia nyanya, pilipili mbichi, pilipili boga, na mchanganyiko uliopunguza awali.
- 🥘 Tia kuku na uchanganye vizuri.
- ⏳ Wakati unakaanga vitunguu ili kuokoa muda, huku chemsha mchele hadi uive nusu kiini, mwaga maji na chuja.
- 🥄 Punguza masala nusu yake na uweke kando.
- 🍚 Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia, na juu yake tena mimina wali.
- 🔥 Funika na upike katika oveni hadi uive.
- 🍽️ Changanya unapopakua katika sahani.
Biriani yako iko tayari! 😋
Maoni