JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🍲
JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🍲
MAHITAJI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🥘
- Njegere – Nusu kilo
- Nazi – 2
- Nyanya – 4
- Karoti – 1
- Pilipili hoho – 1
- Kitunguu maji – 1
- Thoum – Kiasi
- Mafuta ya kupikia – Kiasi
- Chumvi – Kiasi
JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🍲
- Chambua njegere, zikoshe, kisha zitie kwenye sufuria na maji uzichemshe ziive kiasi, lakini zisilainike sana.
- Safisha nyanya, uzimenye na kuzikata. Pia katakata hoho, karoti, na vitunguu. Twanga thoum. Kisha, chujia tui la nazi zito na jepesi.
- Bandika sufuria jikoni, weka mafuta ukaange vitunguu, vikishabadilika rangi tia hoho, kaanga kidogo kisha utie thoum, nyanya, pamoja na karoti, endelea kukaanga.
- Mimina njegere, tia chumvi na mimina tui la nazi jepesi, wacha lichemke. Kisha tia tui la nazi zito liache lichemke kiasi mpaka uzito wa njegere ukiwa sawa, tayari epua.
Enjoy your delicious njegere za nazi! 😋
Maoni