🥗🍗🥙WALI WA KISOMALI NA KUKU
JINSI YA KUPIKA WALI WA KISOMALI NA KUKU
MAHITAJI NA VIPIMO
Vipimo vya Wali 🍚
. Mchele - 3 vikombe
- Vitunguu (viliokatwa vidogo vidogo) - 2
- Mafuta - 3 vijiko vya supu
- Kitunguu saumu (thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
- Bizari ya pilau - 1 kijiko cha supu
- Mdalasini - 1 kijiti
- Hiliki - 3 chembe
- Pilipili manga nzima - chembe chache
- Siagi - 2 vijiko vya supu
- Chumvi - Kiasi
Vipimo vya Kuku 🍗
- Kuku kidari (breast), kata vipande - 2 LB
- Mafuta - 3 vijiko vya supu
- Kitunguu saumu (thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
- Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
- Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo - Kiasi
- Bizari ya pilau (cummin au jiyrah) - 1 kijiko cha chai
- Pilipili kubwa tamu la kijani - 1
- Pilipili kubwa tamu nyekundu - 1 (zikate vipande)
- Karoti iliyokunwa - 1-2
- Chumvi - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali 🍚
- Roweka mchele kwa muda kulingana na aina ya mchele.
- Katika sufuria, tia mafuta na kaanga vitunguu hadi vibadilike rangi kidogo.
- Tia thomu iliyosagwa, mdalasini, bizari ya pilau, hiliki, pilipili manga, na chumvi. Kaanga kidogo.
- Tia mchele, kaanga kwa muda mfupi, kisha tia maji ya moto kulingana na mchele unaotumia.
- Tia siagi, funika, na pika hadi wali uive.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku 🍗
- Mchanganye kuku na thomu/tangawizi iliyosagwa, chumvi, na pilipili mbichi.
- Katika karai, tia mafuta, kisha kaanga kuku na bizari ya pilau (jiyrah).
- Karibu na kuiva, tia vitunguu, pilipili tamu, na kotmiri.
- Kaanga kwa dakika moja tu, uzime moto na epua.
Kupakua
- Pakua wali katika sahani.
- Pambia na karoti iliyokunwa. Unaweza pia kuongeza zabibu ikiwa unapenda.
- Wali na kuku wako tayari kwa kuliwa. 😋
Maoni