KEKI YA ZEBRA
ZEBRA CAKE π¦π° - Keki ya Mistari ya Pundamilia
π MAHITAJI:
β
2 vikombe unga wa ngano πΎ
β
1 kikombe mafuta ya kupikia π’οΈ
β
1 kikombe sukari π§
β
4 mayai π₯
β
1 kikombe maziwa fresh π₯
β
Β½ kijiko cha chai vanilla essence πΏ
β
2 vijiko vikubwa unga wa cocoa π«
β
1 kijiko cha chakula baking powder πΊ
π JINSI YA KUTAYARISHA:
1οΈβ£ Changanya mayai na sukari kwenye bakuli.
Piga hadi mchanganyiko uwe laini na upate povu.
2οΈβ£ Ongeza maziwa na mafuta, endelea kuchanganya hadi vichanganyike vizuri.
3οΈβ£ Tayari mchanganyiko wa unga
Katika bakuli lingine, changanya baking powder, vanilla essence, na unga wa ngano.
Mimina mchanganyiko wa unga kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari.
Changanya hadi upate mchanganyiko laini bila madonge.
4οΈβ£ Gawanya mchanganyiko mara mbili kwenye bakuli mbili zilizo sawa kwa ukubwa.
Nusu moja ibaki ilivyo.
Nusu ya pili ongeza unga wa cocoa na uchanganye vizuri hadi iwe ya rangi ya kahawia.
5οΈβ£ Kutengeneza muundo wa Zebra
Chukua chombo cha kuokea cha mduara kilichopakwa siagi na kunyunyiziwa unga.
Chota kijiko kimoja cha mchanganyiko wa vanilla, mimina katikati ya chombo.
Kisha chota kijiko kimoja cha mchanganyiko wa cocoa, mimina juu ya mchanganyiko wa kwanza.
Rudia hivyo hadi umalize mchanganyiko wote.
6οΈβ£ Oka kwa 180Β°C kwa dakika 35-40 au hadi ukichoma na kijiti kitoke kikavu.
Kama unaoka kwa mkaa, hakikisha moto wa juu na chini ni wa wastani, kama wa kupalilia wali.
7οΈβ£ Baada ya kuiva, acha ipoe kwa dakika 10 ndani ya chombo, kisha itoeni na iache ipoe kabisa kabla ya kukata.
π₯ VIDOKEZO VYA MAFANIKIO:
βοΈ Usitikise chombo baada ya kumimina mchanganyiko ili mistari ya zebra isiharibike.
βοΈ Usisubiri mchanganyiko usambae peke yake, weka kijiko juu ya kingine kwa mpangilio.
βοΈ Usifungue oven mara kwa mara ili keki isishuke.
βοΈ Unaweza kuongeza maziwa kidogo kama mchanganyiko ni mzito sana.
π Furahia Zebra Cake yako yenye muonekano wa kuvutia na ladha tamu! π¦π°
Maoni