JINSI YA KUPIKA VILEJA VYA CHOCOLATE NA VANILLA
JINSI YA KUPIKA VILEJA VYA CHOCOLATE NA VANILLA
MAHITAJI
- 🍚 Unga wa ngano - vikombe 3
- 🥄 Baking soda - 1/2 kijiko cha chai
- 🧂 Chumvi - 1/4 kijiko cha chai
- 🧈 Siagi - kikombe 1
- 🍬 Sukari nyeupe - vikombe 2
- 🥚 Mayai - 2, yalopigwa
- 🍶 Vanilla - kijiko 1 cha chai
- 🍫 Unga wa cocoa (cocoa powder) - 1/4 kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA
1️⃣ Changanya unga pamoja na baking soda na chumvi. Weka pembeni.
2️⃣ Piga siagi na sukari kwa kutumia mchapo au mwiko hadi mchanganyiko uwe mweupe.
3️⃣ Tia mayai na vanilla, kisha piga tena vizuri kuchanganya.
4️⃣ Tia unga kidogo kidogo ukiwa wachanganya hadi ujikusanye na kufanya donge, gawa nusu kwa nusu.
5️⃣ Katika donge moja, tia cocoa (choco primo), kisha changanya vizuri upate donge la chocolate.
6️⃣ Sukuma donge lako la vanilla kufanya umbo la pembe nne, kisha sukuma donge lako la chocolate kuwa umbo la pembe nne pia.
(Kama unga unakusumbua kwa kulainika, weka katika fridge kwa muda wa nusu saa kisha sukuma).
7️⃣ Bebanisha zote mbili, ukianza na donge la vanilla chini na chocolate juu. Sokota kufanya log (kama unakunja busati), kisha zungusha katika plastiki na weka katika fridge hadi iwe set (mgumu).
8️⃣ Washa oven na set joto la 180°C. Funika tray lako la kuokea kwa karatasi ya kuokea au zungusha kwa foil.
(Unaweza pia kupaka tray yako mafuta na kisha kunyunyiza unga).
9️⃣ Toa unga wako kutoka kwenye fridge, kisha kata slices kwa kutumia kisu kikali. Panga katika tray na hakikisha unaacha nafasi kila baada ya kimoja.
🔟 Oka kwa muda wa dakika 10-15 hadi ziset vizuri na kupata rangi pembezoni na chini kwa mbali.
1️⃣1️⃣ Epua, kisha acha zipoe kabisa ndani ya tray.
😋 Furahia vileja vyako vya chocolate na vanilla!
Maoni