JINSI YA KUPIKA BEEF TAMARIND
JINSI YA KUPIKA BEEF TAMARIND
MAHITAJI
- Nyama ya ng'ombe – 1 kg (ikatwa vipande vidogo)
- Chumvi – Kiasi
- Ukwaju – Kiasi
- Beef masala – Kiasi
- Vitunguu thoum – Kiasi
- Pilipili mtama – Kiasi
- Tangawizi – Kiasi
- Mafuta ya kupikia – Kidogo
- Carrot – 1 (kikata vipande vidogo)
- Hoho – 1 (kikata vipande vidogo)
- Vitunguu maji – 2 (vikatwe)
- Pilipili – 2 (zikatwe)
MAELEKEZO:
1️⃣ Andaa nyama ya ng'ombe - Kataa nyama kwa vipande vidogo, osha vizuri na uchuje maji.
2️⃣ Changanya viungo - Tia chumvi, ukwaju, beef masala, vitunguu thoum, pilipili mtama, tangawizi, na mafuta kidogo ya kupikia kwenye nyama.
3️⃣ Weka kwenye fridge - Changanya viungo vyote vizuri na weka nyama kwenye fridge kwa masaa 6 ili viungo vimeng'ane.
4️⃣ Chemsha nyama - Toa nyama kutoka kwenye fridge, weka jikoni na iache icheke mpaka inakaribia kujikaanga yenyewe.
5️⃣ Tia mboga - Ongeza karoti, hoho, vitunguu maji viwili, na pilipili mbili. Acha vichemke kiasi mpaka vikajikaange vyenyewe.
6️⃣ Funika na foil - Ipua nyama, weka mafuta kidogo kwenye kikaango kisha funika kwa foil. Weka kikaango kwenye moto ili moshi usitoke nje.
7️⃣ Pika mpaka iive - Acha nyama ikae kwa muda ili viungo vyote vimeng'ane, kisha funua foil na iache ikae kidogo.
8️⃣ Tayari kwa kuliwa - Nyama inakuwa na ladha ya kimishkaki, sasa iko tayari kuliwa!
Ladha ya Beef Tamarind itakuwa tamu na ya kuvutia, kama mishkaki!
Maoni