JINSI YA KUPIKA UBUYU!!!


JINSI YA KUPIKA UBUYU 



 


MAHITAJI:

  • 🍡 Ubuyu - Kisado
  • 🍚 Ubuyu wa unga
  • 🍬 Sukari - Kilo 2
  • 🌶️ Pilipili manga (ya unga)
  • 🌿 Hiliki (ya unga)
  • 🍦 Vanilla
  • 🎨 Rangi ya ubuyu


MAELEKEZO:

1️⃣ Chambua ubuyu wako na hakikisha hauna takataka yoyote kisha uweke pembeni.
2️⃣ Katika sufuria, weka maji. Acha yapate moto, kisha ongeza sukari, pilipili manga, hiliki, na rangi ya ubuyu. Koroga na acha mchanganyiko uchemke hadi unate (ukinata, basi umeiva).
3️⃣ Mwagia mchanganyiko huo katika ubuyu wa tunda kwa kiasi kidogo kidogo, huku ukiukoroga kwa mwiko ili usiufanye tepetepe.
4️⃣ Ongeza ubuyu wa unga na koroga vizuri mpaka rangi nyeupe ya ubuyu ipotee kabisa.
5️⃣ Acha ubuyu upoe na ukauke. Hakikisha unapooza kwa kuufunika, maana ukipata hewa nyingi utakuwa mgumu.


ANGALIZO:

🔸 Hakikisha mchanganyiko hautoi tepetepe kwa kuumwagia mchanganyiko mwingi mara moja.
🔸 Koroga vizuri kila unapoongeza mchanganyiko ili kuupa ubuyu rangi yake kamili.

😋 Ubuyu wako sasa uko tayari kufurahia!

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUPIKA MIKATE YA CHILA (VIBIBI)

🌿🥩🍌NDIZI ZA NYAMA

VILEJA VYA JICHO LA NGAMIA

🥩🥗🍛BIRIANI YA NYAMA YA NG'OMBE

🍗🥘🍲PILAU YA KUKU

JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🍲

🍪🍯VILEJA VYA CARAMEL

JINSI YA KUPIKA VITUMBUA

🌼🌺VILEJA VYA JAM