πŸ—πŸ₯˜πŸ²PILAU YA KUKU

 NAMNA YA KUPIKA PILAU YA KUKU




VIPIMO

🍚 Mchele wa Mbeya unaonukia - 1 kilo
πŸ— Kuku - 1
πŸ§… Vitunguu - 3
πŸ₯” Viazi/Mbatata - 5
🌿 Jira/Bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
🌰 Mdalasini - 1 kijiti
🌢️ Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
🌟 Hiliki - 3 chembe
πŸͺ΄ Karafuu - 5 chembe
πŸ§„ Kitunguu saumu (thomu/galic) kilichosagwa - 3 vijiko vya supu
πŸ₯„ Tangawizi mbichi iliosagwa - 3 vijiko vya supu
πŸ›’️ Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
πŸ§‚ Chumvi - kiasi


NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1️⃣ Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi, ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu, na tangawizi yote.

2️⃣ Menya viazi na ukate vipande vya kiasi.

3️⃣ Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta kwenye sufuria ya kupikia pilau.

4️⃣ Tia bizari zote isipokuwa hiliki.

5️⃣ Saga hiliki na tia pamoja na kitunguu thomu/somu, kisha ukaange kidogo.

6️⃣ Mimina kuku na supu yake, acha ichemke, kisha tia mchele na viazi.

7️⃣ Koroga vizuri na acha wali uwive katika moto mdogo kama kawaida ya kupika pilau.

πŸ› Pilau yako iko tayari! Furahia chakula chako kitamu. 😊


Maoni