JINSI YA KUPIKA KATLESI ZA NYAMA
Jinsi ya kupika KATLESI za Nyama
mahitaji
-viazi mbatata - Β½
-Nyama ya kusaga robo
-Mayai 3
-Vitunguu maji Vikubwa 2
-pilipili hoho 1
-karoti 1
-Ndimu / limau
-Pilipili manga - kijiko cha chai Β½
-Tangawizi mbichi
-Kitunguu thomu
-Bizari ya mchuzi kijiko cha chai 1
-chumvi kiasi
-Chenga za mkate (Bread crumbs) Weka katika sahani -kikombe 1cha mafuta ya kupikia
Namna ya kupika:
-Menya viazi vikate na uchemshe vikiwa vinakaribia kuiva weka binzari ya manjano, ndimu na chumvi, vitunguu maji, hoho na karoti(iliyokwanguliwa) kisha utaviponda kwa pamoja mpka viwe kama ugali.
-Chemsha Nyama kwa tangawizi na kitunguu thomu, pilipilimanga mpaka ikauke.
- Sasa changanya vizuri na viazi ulivyoviponda ponda na nyama uliyoitia viungo, changanya vizuri mpaka viazi vichanganyike vizuri na nyama.
-Sasa fanya madonge na uviringe kama shepu ya yai au duara kawaida.
-Sasa vunja yale mayai kisha uyakoroge kwenye kibakuli pembeni, baada ya chukua vile viazi vyenye shepu ya duara uvigaragaze kwenye chenga za mkate, vyote viwe vimepakwa chenga za mkate; kisha utachovya kwenye ute wa yai na kuzichoma kwenye mafuta mpaka ziwe na rangi ya dhahabu.
baada ya hapo tayari kuliwa.
NB:- unaweza kutumia nyama ya kuku, au samaki bila kusahau kutoa miba.
-kama hauna chenga za mkate unaweza kutumia unga wa ngano uliochanganywa na sembe kidogo.
-Epuka kugeuza geuza ili zisije zikavurugika kwenye mafuta, na mafuta yawe yamepata moto kiasi kwani zikikaa sana jikoni pia zinaweza kuvurugika.
Maoni