🥗🍗🥙WALI WA TAMBI NA SAUCE YAKE YA KUKU
JINSI YA KUPIKA WALI WA TAMBI NA MCHUZI WAKE WA KUKU
Vipimo Vya Wali 🍚
Vipimo Vya Kuku 🍗
- Kuku kidari (boneless) aliyekatwa katwa vipande - 1 kilo
- Kitunguu maji kilichokatwa katwa - 2
- Kitunguu saumu (thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
- Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
- Chumvi - Kiasi
- Paprika - 1 kijiko cha supu
- Masala ya kuku (tanduri au yoyote) - 1 kijiko cha supu
- Ndimu - 2 vijiko vya supu
- Mtindi (yoghurt) au malai (cream) - 1 kikombe
- Mafuta - ¼ kikombe
- Majani ya kotmiri (coriander) - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali 🍚
- Osha mchele kisha uroweke.
- 🛢️ Tia mafuta katika sufuria, kisha kaanga tambi zilizokatwakatwa hadi zibadilike rangi kuwa nyekundu.
- Tia mchele na endelea kukaanga kwa muda mfupi.
- Tia maji kiasi cha wali kupikika, kama unavyopika pilau (maji yanategemea aina ya mchele).
- 🔥 Funika na pika katika moto mdogo mdogo hadi wali uive.
- Epua ukiwa tayari.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku 🍗
- Katika bakuli, changanya vitu vyote isipokuwa mtindi na kitunguu.
- 🛢️ Tia mafuta katika karai, kisha kaanga kitunguu kwa muda mfupi tu (hakikisha hakigeuki rangi).
- Tia kuku pamoja na masala yake, kisha endelea kukaanga kwa muda.
- 🥛 Tia mtindi au malai, kisha funika na pika hadi kuku aive vizuri.
- 🌿 Nyunyuzia kotmiri iliyokatwakatwa juu ikiwa tayari.
- Tumikia na wali wa tambi kwa ladha ya kipekee! 😋
Maoni