JINSI YA KUPIKA SAGA NOTI

🍯🥮 SAGA NOTI - RECIPE 🥮🍯





🔸 Mahitaji:

1️⃣ Donge la Chumvi 🧂

Unga kiasi 🌾

Hamira 🧫

Chumvi 🧂

Mafuta 🛢️


2️⃣ Donge la Sukari 🍯

Unga kiasi 🌾

Sukari 🍚

Maziwa 🥛

Hamira 🧫

Hiliki 🌿



📝 Jinsi ya Kupika:

1️⃣ Tayarisha madonge
👉 Kanda donge la sukari 🍯 na uache uumuke.
👉 Kanda donge la chumvi 🧂 kisha nalo uache uumuke.

2️⃣ Kukatakata na kusukuma
👉 Kata madonge madogo kiasi ✂️.
👉 Sukuma kama chapati lakini iwe nyembamba (bila kuwa nene sana) 🍽️.
👉 Sukuma kwanza la chumvi, kisha la sukari juu yake ili liwe la mviringo 🔄.

3️⃣ Kuunganisha na kukata
👉 Weka donge la chumvi chini na la sukari juu 🥮.
👉 Iroll vizuri kisha kata vipande vidogo vidogo ⚪ kwa ukubwa unaopenda.

4️⃣ Kupika
👉 Pakaza mafuta 🛢️ na choma kama mandazi 🥯 hadi yawe rangi ya dhahabu.
👉 Chemsha shira (syrup) kisha mwagia juu ili kupata utamu wake wa kipekee 🍯.

🔥 Matokeo ya Mwisho

Sehemu yenye wekundu 🔘 ni unga wa sukari.

Sehemu yenye weupe ⚪ ni unga wa chumvi.


😋

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUPIKA MIKATE YA CHILA (VIBIBI)

🌿🥩🍌NDIZI ZA NYAMA

VILEJA VYA JICHO LA NGAMIA

🥩🥗🍛BIRIANI YA NYAMA YA NG'OMBE

🍗🥘🍲PILAU YA KUKU

JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🍲

🍪🍯VILEJA VYA CARAMEL

JINSI YA KUPIKA VITUMBUA

🌼🌺VILEJA VYA JAM