JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI ZENYE KUCHAMBUKA
JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI ZA KUCHAMBUKA
MAHITAJI
✅Unga wa ngano vikombe 3
✅Samli ilioekwa motoni Kwa sekunde kadhaa vijiko vya mezani takriban
✅Chumvi kiasi chako
✅Maji yasiokuwa moto wala baridi(at room temperature) ukipenda utatumia tuwi ama maziwa.
MATAYARISHO
▪Weka unga kwenye bakuli uchanganye na chumvi vizuri
▪Weka samli uchanganye mpaka vidonge vyote viishe
▪Weka maji kidogo kidogo ukiendelea kukanda unga mpaka ushikane na ulainike vizuri.
▪Funika unga kisha ueke pembeni Kwa takriban dakika 30 au zaidi.
▪Funua unga wako utoe madonge matatu(size ya madonge itategemea na mahali pako pa kusukuma. Kama ni pakubwa unaweza hata ukafanya donge moja Tu)
▪Sukuma donge moja moja kama chapati kisha upake mafuta na ukunje kama swissroll ili kufanya tabaki
▪Gawanya size unayotaka na ukunje vizuri chapati zako
▪Ziwache tena Kwa takriban nusu saa au zaidi ili zizidi kulainika.
▪Bandika chuma cha kuchomea chapati motoni na uache kishike moto
▪Chuma kikiendelea kushika moto, sukuma chapati zako size unayotaka (zisiwe nene wala nyembamba Sana)
▪Chuma kikishashika moto, weka chapati uanze kuchoma
▪Chapati ikishika rangi kidogo upande mmoja,geuza upande wa pili pia ishike rangi
▪Weka samli upande mmoja na uipike chapati Kwa sekunde kadhaa huku ukiikandamiza chini Kwa kitambara au kijiko kikubwa ili ikolee rangi nzuri.
▪Geuza upande wa pili ufanye vivyo hivyo.
▪Kutumia mkono ama kifimbo cha chapati kunja chapati zako mara mbili na uzipige kwa juu.
▪Chapati zipo tayari kuliwa
▪Andaa zikiwa moto kwa maini, maharagwe au chochote upendacho.
Maoni