JINSI YA KUPIKA CAKE ILIYOCHAMBUKA NA VIPIMO VYAKE
Ukitaka kupika cake iliyochambuka vizuri 🍰:
1. Baking powder ichanganye na unga kisha chekecha unga mara mbili au zaidi ili ichanganyanyike vizuri 🧁.
2. Saga sukari na blueband/kimbo/samli mpaka sukari iwe laini kusiwe na machenga chenga na iwe nyeupe na ivimbe ndipo uanze kueka mayai 🧈🍯.
3. Wakati wa KUEKA mayai, weka moja uchanganye kisha jingine hivyo hivyo mpaka yaishe, usieke yote kwa pamoja 🥚.
4. Weka maziwa/maji ya limao au maji ya chungwa katika cake yako (hii inasaidia cake ichambuke sana ndani) 🥛🍋🍊.
5. Wakati wa KUEKA unga, punguza speed ya mashine, ikiwezekana tumia mwiko badala ya mashine kuchanganya unga… na usikoroge kwa muda mrefu, ukishanganyika basi inatosha 🥄.
6. Moto wa kuoka cake usiwe mwingi, cake haitaki moto mwingi, inahitaji joto (mvuke) wa wastani 🌡️.
VIPIMO VYA CAKE
Fata vipimo vya cake hivi👇
Keki
Mayai 12 🥚
Sukari 1/2 🍬
Siagi 1/2 🧈
Unga 1/2 na viganja 2 🍚
Baking powder 2tsp 🧁
Keki
Mayai 10 🥚
Sukari 1/2 🍬
Siagi 1/2 🧈
Unga 1/2 na kiganja 1 🍚
Baking powder 2tsp 🧁
Keki
Mayai 8 🥚
Sukari 1/2 punguza kidogo 🍬
Siagi 1/2 🧈
Unga 1/2 🍚
Baking powder 2tsp 🧁
Keki
Mayai 6 🥚
Sukari 1/4 🍬
Siagi 1/4 🧈
Unga 1/4 🍚
Baking powder 1 tsp 🧁
Maoni