Machapisho

RECIPE ZETU

JINSI YA KUPIKA MAHAMRI/MAANDAZI

Picha
  Mahitaji 🍞 1. Unga wa ngano (tumia unga wa kawaida wa ngano) 🌾 2. Mafuta ya kupikia (kwa kukaanga) 🛢 3. Sukari (kiwango unachopenda, kawaida vijiko 2) 🍬 4. Chumvi kidogo (kidogo tu, ili ladha iwe nzuri) 🧂 5. Hiliki (hiari, lakini inatoa ladha nzuri) 🌿 6. Tuwi la nazi (hii inapatikana kama huna tui, unaweza kutumia mafuta ya kawaida ya kupikia) 🥥 7. Hamira (ni muhimu kwa maandazi kujaa vizuri) 🍞 Hatua za Kupika Maandazi 🍩 1. Changanya Vitu Vyako 🥣: Kwanza, weka unga wa ngano kwenye bakuli kubwa. Ongeza sukari, chumvi kidogo, hiliki (ikiwa unatumia) na hamira. 2. Ongeza Tuwi la Nazi 🥥: Kama unatumia tui la nazi, ongeza kidogo kwenye unga wako ili kutoa ladha nzuri na kufanya maandazi yawe laini.  Kama huna tui la nazi, unaweza kuongeza mafuta kidogo ya kupikia au maji ya kutosha ili kufanya mchanganyiko uwe na unyevu. 3. Kanda Mchanganyiko 🤲: Kanda unga hadi uwe mgumu lakini si ngumu kupitiliza. Hakikisha umechanganya vizuri ili unga uwe laini.  Ukiwa unakanda...

Mini Pizza Recipe 🍕

Picha
  Mini Pizza Recipe 🍕 Ingredients For the pizza crust 400g unga wa kawaida 🍞 2 tsp yeast ya haraka 🌾 1/2 tsp chumvi 🧂 1 tbsp sukari 🍬 1 tbsp maziwa ya unga 🧑‍🍳 1 kikombe cha maji ya moto 💧 2 tbsp mafuta ya zeituni 🫒 For the Devilled Chicken 200g kifua cha kuku (kikate vidogo) 🍗 Pinch ya turmeric 🟡 1/2 tsp chili powder/paprika powder 🌶️ 1 tsp pilipili poda 🌶️ 1 tbsp mafuta ya zeituni 🫒 1 tsp oyster sauce 🦪 1 tsp soya sauce 🍜 1 tsp chumvi 🧂 1 vitunguu vya kati (vilivyo kata nyembamba) 🧅 1/2 tsp ginger garlic paste 🧄 1 tbsp pilipili nyekundu ya kusagwa (kwa wale wapendao pilipili) 🌶️ 1 tbsp mafuta ya sunflower 🌻 Other toppings 1 kikombe Mozarella cheese 🧀 1 kikombe Cheddar cheese 🧀 Pilipili za paprika na peppe/bellpepper za rangi mbili 🌶️🫑 Olives za mweusi zilizokatwa 🫒 Pasta/pizza sauce (ya duka) 🍅 Directions Devilled Chicken : Changanya kuku na viungo (turmeric, chili, pi...

JINSI YA KUPIKA MEATBALLS 🍽️

Picha
  JINSI YA KUPIKA MEATBALLS 🍽️ MAHITAJI 📝 ✅ Nyama iliyosagwa 🥩 ✅ Mazenga (Bread crumbs) 🍞 ✅ Vitunguu maji na vitunguu swaumu 🧄🧅 ✅ Mayai 🥚 ✅ Pilipili kwa apendaye 🌶️ ✅ Mkate 🍞 ✅ Mafuta ya kupikia 🛢️ JINSI YA KUPIKA 👨‍🍳 1️⃣ Chukua kiasi cha nyama iliyosagwa unachopenda. 🥩 2️⃣ Loweka slice mbili za mkate kwenye maji kidogo. 💦 3️⃣ Changanya nyama na mkate uliolowekwa ili zishikane vizuri. 🍞🥩 4️⃣ Katakata vitunguu maji na vitunguu swaumu, kisha ongeza kwenye mchanganyiko. 🧄🧅 5️⃣ Koroga mayai vizuri. 🥚🔄 6️⃣ Tengeneza meatballs kwa kuzifinyanga kwa mikono yako katika umbo la mpira. 🏀 7️⃣ Chovya meatballs kwenye mayai uliyokoroga. 🥚 8️⃣ Pindua meatballs kwenye mazenga (bread crumbs) ili zipate ukoko mzuri. 🍞 9️⃣ Kaanga kwenye mafuta ya moto hadi ziwe na rangi ya kahawia (brown). 🔥🍳 🔟 Toa kwenye mafuta, acha zipowe kidogo, kisha zitumikie. 🍽️😋 👉 Furahia Meatballs zako na kachumbari au sauce upendayo! 😍🍛

🍪 Choco Center Biscuits (Vileja za Chokoleti) Recipe 🍪

Picha
  🍪  Choco Center Biscuits (Vileja za Chokoleti) Recipe  🍪 Biskuti hizi ni laini nje na zina chokoleti tamu iliyoyeyuka ndani! 😍🍫 📌 Mahitaji: ✅ Kwa Biskuti: 🍚 2 ½ vikombe unga wa ngano 🍬 ½ kikombe sukari ya unga (icing sugar) 🌿 1 tsp vanilla essence 🥄 1 tsp baking powder 🧈 ½ kikombe siagi (butter) 🥛 1/3 kikombe maziwa ya maji au fresh cream 🥚 1 yai ✅ Kwa Kujaza Ndani: 🍫 100g chokoleti (ya maziwa au dark chocolate, iliyokatwa vipande vidogo) 🥄 2 tbsp maziwa (kwa kuyeyusha chokoleti) 📝 Jinsi ya Kutayarisha: 1️⃣ Tayarisha Ujazo wa Chokoleti: 🔥 Chemsha maji kidogo kwenye sufuria kisha weka bakuli juu yake (double boiler method). 🍫 Weka vipande vya chokoleti na maziwa kwenye bakuli, kisha uyeyushe hadi iwe laini. ❄️ Acha ipoe kidogo na iwe nzito. Unaweza kuihifadhi kwenye friji dakika 10. 2️⃣ Kutengeneza Mchanganyiko wa Biskuti: 🧈 Changanya siagi na sukari ya unga hadi iwe laini na chepesi. 🥚 Ongeza yai na vanilla, ...

JINSI YA KUPIKA MKATE WA MAYAI 🥚🍞

Picha
VITU UNAVYOHITAJI 📝 ✅ Mayai – 4 🥚🥚🥚🥚 ✅ Sukari – ¼ kikombe 🍚 ✅ Unga wa ngano – Vijiko 5 ½ vya chakula 🌾 ✅ Hiliki ya kusaga – ½ kijiko cha chai 🌿 ✅ Baking powder – ½ kijiko cha chai 🎂 ✅ Zabibu kavu – ¼ kikombe 🍇 NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 👩‍🍳🔥 1️⃣ Katika bakuli, weka sukari na hiliki, kisha vunja mayai yote manne juu yake. 🥚🍚 2️⃣ Tumia mashine ya kukorogea keki au whisk kupiga mchanganyiko mpaka sukari iyeyuke na mayai yaumuke. 🔄🥄 3️⃣ Washa oven yako kwa 350°F (175°C) ili ipate moto mapema. 🔥 4️⃣ Changanya baking powder na unga wa ngano kisha uanze kuuongeza kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari. Hakikisha unakoroga vizuri ili usiwe na madonge. 🍞 5️⃣ Mimina mchanganyiko kwenye sufuria ya kuchomea keki, kisha nyunyizia zabibu kavu juu yake. 🍇 6️⃣ Ingiza sufuria kwenye oven na uoke kwa dakika 20. ⏳🔥 7️⃣ Angalia kama mkate umeiva kwa kuchoma kijiti katikati – kikitoka kikiwa kikavu, mkate umeiva! 📌✅ 8️⃣ Ikiwa bado mbichi, rudish...

JINSI YA KUTENGENEZA SPRING ROLLS 🌯🔥

Picha
JINSI YA KUTENGENEZA SPRING ROLLS 🌯🔥 Spring Rolls ni kitafunwa kitamu kinachoweza kuliwa na kinywaji chochote—cha moto au baridi. Hutengenezwa kwa kutumia manda (kama zile za sambusa) na hujazwa nyama ya kusaga au mboga kisha kufungwa katika umbo la silinda kabla ya kukaangwa kwenye mafuta. Hapa nitakuelekeza jinsi ya kuzitengeneza. 📌 MAHITAJI ✅ Nyama ya kusaga – 1kg 🥩 ✅ Manda – Karatasi 30 (umbo la mraba) 🫓 ✅ Vitunguu maji – 4 vikubwa 🧅 ✅ Karoti – 4 kubwa 🥕 ✅ Chumvi – 1 kijiko cha chai 🧂 ✅ Tangawizi na kitunguu saumu (iliyopondwa) – 1 kijiko kikubwa 🧄 ✅ Mafuta ya kupikia – 1 lita 🛢️ 📝 JINSI YA KUTENGENEZA 1️⃣ Kuandaa nyama Osha nyama ya kusaga na uiweke kwenye chujio. Mimina kwenye frying pan bila kuongeza mafuta, kwa sababu nyama ina mafuta yake. Acha iive hadi maji yakauke, kisha ongeza karoti, vitunguu, kitunguu saumu na tangawizi . Endelea kukaanga hadi kila kitu kiwe tayari, kisha ipoe. 2️⃣ Kufunga Spring Rolls Chukua manda moja, weka kijiko 1 k...

VIPIMO VYA MKATE WA MAYAI

Picha
VIPIMO VYA MKATE WA MAYAI Mkate Mayai 12 🥚 Sukari 1/4 🍬 Unga 1/4 🍞 Baking powder 1tbsp 🧁 Hiliki na vanilla extract 🌿🍦 Mkate Mayai 10 🥚 Sukari 1/4 🍬 Unga 1/4 🍞 Baking powder, hiliki na vanilla extract 🧁🌿🍦 Mkate Mayai 8 🥚 Sukari 1/4 🍬 Unga 1/4 🍞 Baking powder, hiliki na vanilla extract 🧁🌿🍦 Mkate Mayai 6 🥚 Sukari 1/4 punguza kidogo 🍬 Unga 1/4 🍞 Baking powder, hiliki na vanilla extract 🧁🌿🍦 KIDOKEZO Ktk mkate wa mayai, ikiwa mayai ni 12 utatia unga vijiko vya kulia 12, km mayai 10 utatia unga vijiko 10, km mayai 8 utatia unga vijiko 8, na km mayai 6 utatia unga vijiko 6. ✨ For a good result, follow these instructions! 👍

JINSI YA KUPIKA CAKE ILIYOCHAMBUKA NA VIPIMO VYAKE

Picha
JINSI YA KUPIKA CAKE ILIYOCHAMBUKA NA VIPIMO VYAKE Ukitaka kupika cake iliyochambuka vizuri 🍰: 1. Baking powder ichanganye na unga kisha chekecha unga mara mbili au zaidi ili ichanganyanyike vizuri 🧁. 2. Saga sukari na blueband/kimbo/samli mpaka sukari iwe laini kusiwe na machenga chenga na iwe nyeupe na ivimbe ndipo uanze kueka mayai 🧈🍯. 3. Wakati wa KUEKA mayai, weka moja uchanganye kisha jingine hivyo hivyo mpaka yaishe, usieke yote kwa pamoja 🥚. 4. Weka maziwa/maji ya limao au maji ya chungwa katika cake yako (hii inasaidia cake ichambuke sana ndani) 🥛🍋🍊. 5. Wakati wa KUEKA unga, punguza speed ya mashine, ikiwezekana tumia mwiko badala ya mashine kuchanganya unga… na usikoroge kwa muda mrefu, ukishanganyika basi inatosha 🥄. 6. Moto wa kuoka cake usiwe mwingi, cake haitaki moto mwingi, inahitaji joto (mvuke) wa wastani 🌡️. VIPIMO VYA CAKE Fata vipimo vya cake hivi👇 Keki Mayai 12 🥚 Sukari 1/2 🍬 Siagi 1/2 🧈 Unga 1/2 na viganja 2 🍚 Baking powder 2tsp 🧁 Keki ...

MATATIZO YA MUONEKANO WA KEKI 🎨

Picha
MATATIZO YA MUONEKANO WA KEKI 🎨 🟠 SUALA LA 7: SEHEMU ZA JUU ZA KEKI HAZIKUPATA RANGI NZURI 🎭 ✅ Keki haikuwekwa katikati ya oven 📍 ✅ Viwaya vya oven havipo sawa – hakikisha treya iko katikati ⚖️ 🟠 SUALA LA 8: KEKI IMEUNGUA 🔥 ✅ Moto mwingi juu = imeungua juu 🔝❌ ✅ Moto mwingi chini = imeungua chini 🔻❌ MATATIZO YA NJE YA KEKI 🌍 🟠 SUALA LA 9: NJE YA KEKI IPO MAJI MAJI NA INANG’ATA 🫠 ✅ Sukari au siagi/margarine nyingi sana 🧈🥄 ✅ Unga usiofaa kwa kuoka keki 🌾 ✅ Umeacha keki kwenye treya kwa muda mrefu – hamishia kwenye cooling rack! 🛖 🟠 SUALA LA 10: SEHEMU YA NJE YA KEKI IMETENDA GAMBA GUMU 🏏 ✅ Moto wa oven ulikuwa mkubwa sana au mdogo sana 🔥 ✅ Umezidisha sukari au mayai kwenye upishi 🍳 🟠 SUALA LA 11: KEKI IMEPASUKA PASUKA JUU 😬 ✅ Moto wa juu ulikuwa mwingi 🔝🔥 ✅ Mchanganyiko ulikuwa mzito – ongeza majimaji kidogo 🥛 MATATIZO YA NDANI YA KEKI 🏠 🟠 SUALA LA 12: SEHEMU YA NDANI YA KEKI IPO MAJIMAJI KAMA SIMA 🍵 ✅ Sukari nyingi kupita kiasi 🥄❌ ✅ Keki haijaiva –...

MASWALI MBALI MBALI JUU YA UPISHI WA KEKI 🍰🎂

Picha
MASWALI MBALI MBALI JUU YA UPISHI WA KEKI 🍰🎂 Tunazingatia matatizo yanayotokea wakati wa kuoka keki (hata mkate wa mayai ni keki! 😉). Tambua kosa lako na ujirekebishe! MATATIZO YA KEKI KUUMUKA 🧁 🟠 SUALA LA 1: KEKI HAIKUUMUKA AU IMEUMUKA KIDOGO TU Sababu zake: ✅ Baking powder au chachu ya kuumua keki: Umesahau kuiweka? 😱 Umetia kidogo sana? 👎 Baking powder ime-expire? 🕰️ Haijaexpire lakini imeharibika kwa kuhifadhiwa vibaya? 🔄 ✅ Mchanganyiko haujachanganywa vizuri Usichanganye sana wala kidogo mno. Hakikisha mahitaji yamechanganyika vya kutosha. 🌀 ✅ Moto wa oven ulikuwa mdogo Hakikisha oven imepata joto sahihi kabla ya kuweka keki. ⚡🔥 Usifungue mlango wa oven mara kwa mara! 🚪❌ ✅ Mahitaji ya majimaji yalizidi au yalikuwa machache Fuata vipimo sahihi, usikisie! 📏🥛 ✅ Unga, siagi/margarine havifai kwa kuoka keki Tumia bidhaa zilizoandikwa ‘SUITABLE FOR BAKING’ 🏷️ ✅ Umetumia chombo kikubwa mno kwa kiasi cha mchanganyiko Tumia saizi inayoshauriwa kwenye recipe 📏 ✅ ...

KEKI YA ZEBRA

Picha
ZEBRA CAKE 🦓🍰 - Keki ya Mistari ya Pundamilia 📌 MAHITAJI: ✅ 2 vikombe unga wa ngano 🌾 ✅ 1 kikombe mafuta ya kupikia 🛢️ ✅ 1 kikombe sukari 🧂 ✅ 4 mayai 🥚 ✅ 1 kikombe maziwa fresh 🥛 ✅ ½ kijiko cha chai vanilla essence 🌿 ✅ 2 vijiko vikubwa unga wa cocoa 🍫 ✅ 1 kijiko cha chakula baking powder 🏺 📝 JINSI YA KUTAYARISHA: 1️⃣ Changanya mayai na sukari kwenye bakuli. Piga hadi mchanganyiko uwe laini na upate povu. 2️⃣ Ongeza maziwa na mafuta, endelea kuchanganya hadi vichanganyike vizuri. 3️⃣ Tayari mchanganyiko wa unga Katika bakuli lingine, changanya baking powder, vanilla essence, na unga wa ngano. Mimina mchanganyiko wa unga kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari. Changanya hadi upate mchanganyiko laini bila madonge. 4️⃣ Gawanya mchanganyiko mara mbili kwenye bakuli mbili zilizo sawa kwa ukubwa. Nusu moja ibaki ilivyo. Nusu ya pili ongeza unga wa cocoa na uchanganye vizuri hadi iwe ya rangi ya kahawia. 5️⃣ Kutengeneza muundo wa Zebra Chukua chombo cha kuokea cha mduar...

🥖 JINSI YA KUTENGENEZA MIKATE YA MOFA

Picha
🥖 JINSI YA KUTENGENEZA MIKATE YA MOFA 🥖 📌 Mahitaji ✅ 2 vikombe vya unga wa ngano 🌾 ✅ ½ kikombe cha unga wa sembe 🌽 ✅ 1 tsp ya chumvi 🧂 ✅ 3 tbsp za sukari 🍚 ✅ 1 tsp ya baking powder 🥄 ✅ 1 tbsp ya hamira (yeast) 🍞 ✅ 2 vikombe vya maji ya uvuguvugu 💦 ✅ Mafuta kwa kupikia 🛢️ ✅ Kitunguu saumu kilichosagwa (hiari)🧄 📝 Jinsi ya Kutayarisha 1️⃣ Tengeneza mchanganyiko – Chukua bakuli kubwa, changanya unga wa ngano, unga wa sembe, chumvi, sukari, baking powder, na hamira. Koroga vizuri ili viambato vichanganyike. 2️⃣ Ongeza maji – Mimina maji ya uvuguvugu kidogo kidogo huku ukichanganya. Endelea kuchanganya hadi upate mchanganyiko mzito kama wa mkate wa ufuta au kaimati. Kama una mashine ya kuchanganya keki, unaweza kuitumia kupata mchanganyiko laini zaidi. 3️⃣ Uache uumuke – Funika bakuli na uache mchanganyiko uumuke hadi uongezeke maradufu. 4️⃣ Pasha chuma cha mikate – Weka chuma cha kupikia mikate jikoni na kipate moto, kisha paka mafuta kido...

🥥 NJUGU MAWE ZA TUI LA NAZI 🥜

Picha
🥥 NJUGU MAWE ZA TUI LA NAZI 🥜 📌 MAHITAJI ✅ 250g (robo kilo) njugu mawe 🌰 ✅ 1 nazi 🥥 ✅ 10 punje za hiliki 🌿 ✅ 5 vijiko vya chakula sukari 🍚 ✅ 1 kijiko cha chakula custard powder ✨ ✅ 1 kijiko cha chai arki (vanilla) 🌼 ✅ Chumvi kidogo 🧂 📝 MAANDALIZI 1️⃣ Chagua njugu mawe zako – Ondoa mawe na uchafu wote. 2️⃣ Osha vizuri – Zisuuze kwa maji safi kisha weka kwenye chombo. 3️⃣ Tayarisha tui – Kata nazi yako na kamua tui: Tui zito (kikombe kidogo cha chai) Tui jepesi (kibakuli kimoja) 4️⃣ Menya na twanga hiliki – Changanya na sukari kidogo ili ipate harufu nzuri. 5️⃣ Changanya custard – Katika tui zito, changanya custard powder na weka pembeni. 👨‍🍳 JINSI YA KUPIKA 1️⃣ Chemsha njugu – Weka njugu kwenye sufuria na maji kiasi. Pika kwa moto mdogo huku ukiweka maji kidogo kidogo hadi ziive vizuri. 2️⃣ Ongeza tui jepesi – Mimina tui jepesi, hiliki iliyosagwa, sukari, na chumvi. Acha ichemke hadi tui lipungue. 3️⃣ Mimina tui zito na arki – Ongeza tui zito lililochanganywa na ...

JINSI YA KUPIKA MEATROLLS

Picha
🥐JINSI YA KUPIKA MEATROLL TAMU 📌 MAHITAJI ✅ 1 kikombe siagi 🧈 ✅ 2 vikombe unga wa ngano 🌾 ✅ Maji kiasi 💧 ✅ 1 kikombe nyama ya kusaga 🥩 ✅ ½ kijiko cha chai pilipili manga ya unga 🌶️ ✅ ½ kijiko cha chai kitunguu saumu (thomu) iliyosagwa 🧄 ✅ ½ kijiko cha chai tangawizi iliyosagwa 🌱 ✅ Chumvi kiasi 🧂 📝 JINSI YA KUTAYARISHA 1️⃣ Pika nyama – Changanya nyama, pilipili manga, thomu, tangawizi na chumvi ndani ya sufuria. Pika bila mafuta wala maji, huku unaikoroga koroga hadi iwe kavu. Epua na weka pembeni. 2️⃣ Tengeneza unga – Changanya unga na siagi hadi uchanganyike vizuri. Ongeza maji kiasi ili ushikane, lakini usiukande sana. 3️⃣ Sukuma na kata – Kata madonge na usukume kama unavyotengeneza chapati, lakini usiufanye mwembamba sana. Kata vipande virefu (rectangular). 4️⃣ Funga nyama – Weka nyama juu ya kila kipande cha unga. Kunja upande mmoja kufunika nyama. Kunja upande wa pili kufunika sehemu ya kwanza. 5️⃣ Tengeneza nakshi – Tumia uma kuchoma choma juu ya meat roll...

🧆🔥 JINSI YA KUPIKA BAGIA ZA DENGU 🔥🧆

Picha
  🧆🔥  JINSI YA KUPIKA BAGIA ZA DENGU  🔥🧆 📌 Mahitaji: 🥣 Unga wa dengu – 3 vikombe vikubwa 🧂 Chumvi – 1 kijiko cha chai 💧 Maji baridi – 1 glasi 🌟 Baking powder – 1 kijiko cha chai 🌿 Majani ya kotmiri yaliyokatwakatwa – kiasi 🧅 Kitunguu maji kiliosagwa – 2 vijiko vya supu 🧄 Kitunguu saumu (thomu) kiliosagwa au unga – 1 kijiko cha chai 🛢️ Mafuta – kiasi cha kutosha kwa kukaanga 📝 Jinsi ya Kutayarisha na Kupika: 1️⃣ Kuandaa mchanganyiko 🔹 Katika bakuli lenye nafasi, mimina unga wa dengu na viungo vyote. 🔹 Tumia uma au kijiko kuvuruga mpaka upate mchanganyiko laini bila mabonge. 🔹 Hakikisha si mzito sana wala mwembamba sana. 🔹 Acha mchanganyiko upumzike kwa dakika 15-20 ⏳. 2️⃣ Kukaanga Bagia 🔥 Weka karai au sufuria nzito jikoni, mimina mafuta na acha yapate moto vizuri. 🥄 Tumia kijiko cha chakula kuchota mchanganyiko na mimina kwa uangalifu kwenye mafuta. 🔄 Geuza bagia upande wa pili hadi ziive na kupata rangi ya kahawia mpau...

JINSI YA KUPIKA KATLESI ZA NYAMA

Picha
Jinsi ya kupika KATLESI za Nyama mahitaji -viazi mbatata - ½ -Nyama ya kusaga robo -Mayai 3 -Vitunguu maji Vikubwa 2  -pilipili hoho 1 -karoti 1 -Ndimu / limau  -Pilipili manga - kijiko cha chai ½ -Tangawizi mbichi  -Kitunguu thomu  -Bizari ya mchuzi kijiko cha chai 1  -chumvi kiasi -Chenga za mkate (Bread crumbs) Weka katika sahani -kikombe 1cha mafuta ya kupikia Namna ya kupika : -Menya viazi vikate na uchemshe vikiwa vinakaribia kuiva weka binzari ya manjano, ndimu na chumvi, vitunguu maji, hoho na karoti(iliyokwanguliwa) kisha utaviponda kwa pamoja mpka viwe kama ugali. -Chemsha Nyama kwa tangawizi na kitunguu thomu, pilipilimanga mpaka ikauke.  - Sasa changanya vizuri na viazi ulivyoviponda ponda na nyama uliyoitia viungo, changanya vizuri mpaka viazi vichanganyike vizuri na nyama. -Sasa fanya madonge na uviringe kama shepu ya yai au duara kawaida. -Sasa vunja yale mayai kisha uyakoroge kwenye kibakuli pembeni, baada ya chukua vile viazi...

JINSI YA KUPIKA KAIMATI

Picha
JINSI YA KUPIKA KAIMATI/KALIMATI MAHITAJI 🟠Ngano vikombe v4 yani nusu 🟠Maziwa yauga vijiko v4 🟠Maziwa ya maji kikombe k1 na nusu/ tui la nazi  🟠Hamira kijiko k1  🟠Sukari kikombe k1 🟠Vanila kijiko ki1 🟠Radha ya maziwa kijiko cha chai 🟠Yai 1 🟠Hiliki kijiko k1 🟠Maziwa mgando  🟠Baking p kijiko cha chai 🟠chumvi kijiko cha chai Namna ya kuanda Chuja unga wako vizuri  Weka hamir,chumvi,sukari,yai,maziwa mgando,maziwa ya unga,baking powder na yai changanya vyote kwa p1 Weka maji  Anza kuchanganya kwa kuupiga piga mpaka ulainike vzr Funika vzr kwa muda wa lisaa li1 uumuke Bandika mafuta jikoni kwa moto mdogo dogo anza kuweka kalmati zako kor oga ili kupata rangi inayo fanana Kama unavyoona kweny video Namna ya kuandaa shira Weka maji  kikombe ki 1kweny sufulia weka sukari na hiliki Bandika jikoni uku ukiikoroga mpk ianze kutoa povu na kua nzito inayo nata  Kama unavyoona kwenye video Imimine kwenye bakuli ulilo weka kalmat zako na anza k...

JINSI YA KUPIKA SAGA NOTI

Picha
🍯🥮 SAGA NOTI - RECIPE 🥮🍯 🔸 Mahitaji: 1️⃣ Donge la Chumvi 🧂 Unga kiasi 🌾 Hamira 🧫 Chumvi 🧂 Mafuta 🛢️ 2️⃣ Donge la Sukari 🍯 Unga kiasi 🌾 Sukari 🍚 Maziwa 🥛 Hamira 🧫 Hiliki 🌿 📝 Jinsi ya Kupika: 1️⃣ Tayarisha madonge 👉 Kanda donge la sukari 🍯 na uache uumuke. 👉 Kanda donge la chumvi 🧂 kisha nalo uache uumuke. 2️⃣ Kukatakata na kusukuma 👉 Kata madonge madogo kiasi ✂️. 👉 Sukuma kama chapati lakini iwe nyembamba (bila kuwa nene sana) 🍽️. 👉 Sukuma kwanza la chumvi, kisha la sukari juu yake ili liwe la mviringo 🔄. 3️⃣ Kuunganisha na kukata 👉 Weka donge la chumvi chini na la sukari juu 🥮. 👉 Iroll vizuri kisha kata vipande vidogo vidogo ⚪ kwa ukubwa unaopenda. 4️⃣ Kupika 👉 Pakaza mafuta 🛢️ na choma kama mandazi 🥯 hadi yawe rangi ya dhahabu. 👉 Chemsha shira (syrup) kisha mwagia juu ili kupata utamu wake wa kipekee 🍯. 🔥 Matokeo ya Mwisho Sehemu yenye wekundu 🔘 ni unga wa sukari. Sehemu yenye weupe ⚪ ni unga wa chumvi. 😋

JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI ZENYE KUCHAMBUKA

Picha
JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI ZA KUCHAMBUKA        MAHITAJI ✅Unga wa ngano vikombe 3 ✅Samli ilioekwa motoni Kwa sekunde kadhaa vijiko vya mezani takriban  ✅Chumvi kiasi chako ✅Maji yasiokuwa moto wala baridi(at room temperature) ukipenda utatumia tuwi ama maziwa. MATAYARISHO ▪Weka unga kwenye bakuli uchanganye na chumvi vizuri ▪Weka samli uchanganye mpaka vidonge vyote viishe ▪Weka maji kidogo kidogo ukiendelea kukanda  unga mpaka ushikane na ulainike vizuri. ▪Funika unga kisha ueke pembeni Kwa takriban dakika 30 au zaidi. ▪Funua unga wako utoe madonge matatu(size ya madonge itategemea na mahali pako pa kusukuma. Kama ni pakubwa unaweza hata ukafanya donge moja Tu) ▪Sukuma donge moja moja kama chapati kisha upake mafuta na ukunje kama swissroll ili kufanya tabaki ▪Gawanya size unayotaka na ukunje vizuri chapati zako ▪Ziwache tena Kwa takriban nusu saa au zaidi ili zizidi kulainika. ▪Bandika chuma cha kuchomea chapati motoni na uache kishike moto...

NDIZI ZA NAZI NA SAMAKI

Picha
JINSI YA KUPIKA NDIZI ZA SAMAKI Viungo: ✅ Ndizi mbichi - 6 (zikatwe vipande vikubwa) ✅ Samaki - ½ kg (unaweza kutumia samaki mzima au vipande) ✅ Tui la nazi - vikombe 2 (kikombe 1 cha tui zito na 1 la tui jepesi) ✅ Kitunguu maji - 1 kubwa (kimenyewe na kukatwa vipande vidogo) ✅ Nyanya - 2 (zilizosagwa au kupondwa) ✅ Hoho - 1 (ikakatwa vipande vidogo) ✅ Tungule (kitunguu saumu) - punje 3 (zilizosagwa) ✅ Tangawizi - kijiko 1 cha chai (imepondwa) ✅ Pilipili mbuzi (si lazima) - 1 au 2 ✅ Chumvi - kiasi cha ladha ✅ Mafuta ya kupikia - kijiko 1 cha chakula ✅ Bizari ya manjano (turmeric) - ½ kijiko cha chai ✅ Pilipili manga - ½ kijiko cha chai ✅ Maji - kikombe 1 (kama itahitajika) ✅ Mbaazi au njegere za nazi (si lazima) Maelekezo ya Kupika: 1️⃣ Kuandaa samaki. Osha samaki vizuri na upake chumvi kidogo, bizari ya manjano, na pilipili manga. Mkaange kidogo kwa mafuta mpaka iwe rangi ya kahawia au unaweza kuchemsha kwa chumvi kidogo. Weka pembeni. 2️⃣ Kuandaa ndizi. Menya ndizi na zikate vipande ...

Mikate ya Ufuta Recipe 🍞

Picha
  Mikate ya Ufuta Recipe  🍞 Mahitaji: Vikombe 3 vya unga 🍚 Vijiko 2 vya chai ya yeast 🍞 Vikombe 2 1/2 vya tuwi la nazi 🥥 Nusu kikombe cha mbegu za ufuta 🌰 Vijiko 2 vya yogurt (hiari) 🍶 Nusu kijiko cha #Sunsalt (chumvi) 🧂 Yai 1 (la ukubwa wa kati) 🥚 Siagi au margarine kwa kupaka 🧈 Kwenye kupika mikate ya ufuta ni vizuri kuwa na pan kuanzia mbili, hii itakupa urahisi wa kupika pishi hili.   Namna ya Kutayarisha: 1. Changanya unga na chumvi, yai, na yeast. Ongeza tuwi la nazi na yogurt kisha koroga mpaka mchanganyiko uwe wa kuvuta (utakuwa na texture ya mvuto). 2. Funika mchanganyiko na uache upandishe mpaka ukubwa wake uongezeke mara mbili. Ikiwa unataka ladha ya kipekee, unaweza kuacha inavyoongezeka mara mbili. 3. pasha pan ya kupikia kwa moto wa kati, kisha nyunyiza maji ya chumvi na mimina mchanganyiko kiasi juu yake. Tumia mikono yako kusambaza mchanganyiko kwa unene wa nusu inchi. 4. Nyunyiza mbegu za ufuta juu ya mchanganyiko na acha kwa dakika 3 hadi 4. 5....

Pilau ya Samaki 🐟🍛

Picha
Pilau ya Samaki 🐟🍛 📝 Mahitaji: ✅ Kwa Samaki na Viazi: 🐟 Vipande 4 vya samaki (vipande vikubwa) 🥔 Viazi 8 (menya, osha, na kata vipande vikubwa) 🌶️ Pilipili hoho ya njano 1 (kata vipande) 🧅 Kitunguu kikubwa 1 (kata vipande) 🧄 1/4 kijiko cha chai cha pilipili manga 🧂 1/4 kijiko cha chai cha chumvi ya kitunguu saumu 🥄 1 kijiko cha chai cha mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu saumu 🛢️ Mafuta ya kukaangia 🧂 Chumvi kwa ladha ✅ Kwa Wali: 🍚 Vikombe 3 vya mchele (uoshe vizuri) 🧅 Kitunguu 1 (kata vipande) 🛢️ Mafuta 🥄 1 kijiko cha chakula cha mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu saumu 🌿 Viungo: 🥄 1 kijiko cha chakula cha binzari nyembamba (cumin) 🌰 3 iliki ⚫ 1/2 kijiko cha chai cha pilipili manga 🌿 1 kijiti cha mdalasini 💦 Maji ya moto 👨‍🍳 Jinsi ya Kupika: 🔹 Hatua ya 1: Kuandaa na Kukaanga Samaki 1️⃣ Mchanganye samaki na chumvi, pilipili manga, na chumvi ya kitunguu saumu, kisha acha kwa dakika chache ili viungo viingie vizuri. 2️⃣ Weka mafuta kw...

MUHOGO WA NAZI NA SAMAKI 🥥🐟

Picha
  JINSI YA KUPIKA MUHOGO WA NAZI NA SAMAKI  🥥🐟 📝 Mahitaji: ✅ Kwa Mihogo: Mihogo – 4 vipande Tui la nazi – 2 vikombe Chumvi – ½ kijiko cha chai Maji – 1 ½ kikombe (ikiwa inahitajika) ✅ Kwa Samaki: Samaki – 2 wakubwa (aina yoyote upendayo) Chumvi – 1 kijiko cha chai Ndimu/Limao – 1 kubwa Pilipili manga – ½ kijiko cha chai Kitunguu swaumu – 1 kijiko cha chai (iliyopondwa) Tangawizi – 1 kijiko cha chai (iliyopondwa) Mafuta – ya kukaangia ✅ Kwa Mapambo: Kachumbari (nyanya, kitunguu na pili pili hoho) Limao/ndimu (kwa kuongeza ladha) 👨‍🍳 Jinsi ya Kupika: 🔹 Hatua ya 1: Kupika Mihogo ya Nazi 1️⃣ Menya mihogo na ikate vipande vidogo vidogo. 2️⃣ Chemsha mihogo kwenye sufuria kwa dakika 10 ikiwa unatumia gesi. 3️⃣ Kamua tui la nazi kisha mimina kwenye mihogo iliyokuwa inachemka. 4️⃣ Ongeza chumvi kidogo na acha vitokote kwa dakika 10 nyingine ili nazi iive vizuri. 5️⃣ Bonyeza mihogo kwa mwiko ili uhakikishe imelainika. Ikiwa bado ni ngumu, ongeza maji kidogo n...