Unga wa ngano – 2 vikombe
Siagi (au margarine) – 1 kikombe (iwe laini)
Sukari – ¾ kikombe
Yai – 1
Vanilla – 1 kijiko cha chai
Nazi – 1 kikombe
Baking powder – 1 kijiko cha chai
Chumvi – kiasi kidogo
Jamu (aina yoyote unayopenda: strawberry, raspberry, nk)
Namna ya Kupika
1. Piga siagi na sukari hadi mchanganyiko uwe mweupe na laini.
2. Ongeza yai na vanilla, endelea kuchanganya hadi ichanganyike vizuri.
3. Katika bakuli tofauti, changanya unga wa ngano, baking powder, na chumvi.
4. Changanya unga taratibu ndani ya mchanganyiko wa siagi.
5. Ongeza nazi iliyokunwa na koroga kwa mkono au mwiko hadi ipate donge.
6. Chukua kiasi kidogo cha donge, tengeneza duara, kisha weka kwenye treya ya kuokea (ambayo imepakwa mafuta au imewekwa karatasi ya kuokea).
7. Tumia kijiko kidogo kubonyeza katikati ya kila kiduara (ili kutengeneza nafasi kwa jam).
8. Weka kijiko kidogo cha jamu kwenye kila nafasi ya katikati.
9. Oka kwenye oveni iliyowashwa moto wa 180°C kwa dakika 12–15, au hadi biskuti zibadilike rangi kuwa za kahawia ya dhahabu kwenye kingo.
10. Zipoe kabisa kabla ya kuzihifadhi au kula.
Maoni