Mahitaji (kwa takribani biskuti 15–20).
200g siagi (butter), laini ya chumbani
100g sukari ya kawaida (caster sugar)
300g unga wa ngano (plain flour)
Kiasi kidogo cha chumvi (hiari)
Vifaa vinavyohitajika.
Bakuli kubwa
Mchanganyiko wa mikono au mashine ya kuchanganya
Roller (kipuli)
Kikata biskuti au glasi
Trei ya kuokea
Oveni
Hatua kwa Hatua za Kupika.
✍️Tayari siagi yako inapaswa kuwa laini (room temperature). Pima na uweke viambato vyote tayari.
✍️Katika bakuli kubwa, weka siagi na sukari, halafu changanya vizuri hadi mchanganyiko uwe mwepesi, mweupe na laini (creamy). Unaweza kutumia mashine au mikono.
✍️Weka unga kidogo kidogo kwenye mchanganyiko huo wa siagi na sukari. Koroga hadi mchanganyiko utengeneze donge (dough) linaloshikamana vizuri.
✍️Funika donge na uliweke kwenye friji kwa dakika 20–30 ili likaze kidogo na kuwa rahisi kukata
✍️Toa donge kwenye friji, lisukume kwa roller hadi liwe na unene wa takribani 1 cm. Kata umbo la duara au lolote unalopendelea kwa kutumia kikata biskuti au glasi.
✍️Panga biskuti zako kwenye trei ya kuokea iliyopakwa karatasi ya kuokea (baking paper). Acha nafasi kidogo kati ya kila biskuti. Unaweza kuchoma kwa uma ili kuongeza muonekano kama kwenye picha.
✍️Washa oveni mapema kwenye nyuzi joto 160°C (320°F). Oka biskuti kwa dakika 15–20 hadi ziwena rangi ya dhahabu iliyofifia pembeni.
✍️Toa kwenye oveni na acha zipoe kwenye trei kwa dakika chache kabla ya kuhamishia kwenye wire rack zipoe kabisa.
Vidokezo Muhimu✍️✍️
Usizichome sana biskuti, zinapaswa kuwa nyepesi na laini.
Unaweza kuongeza vanilla au zest ya limao kwa ladha zaidi.
Hifadhi kwenye chombo kisichopitisha hewa kwa siku kadhaa.
Maoni