🌾 MAPISHI YA UJI WA MTAMA MZIMA
🌾 MAPISHI YA UJI WA MTAMA MZIMA
📌 Mahitaji:
Mtama mzima (tayari umeoshwa) – kikombe 1
Maji – vikombe 5 au zaidi (kutegemea uhitaji)
Chumvi kidogo sana 🧂
Siagi – kijiko 1 cha chakula (optional lakini inapendeza) 🧈
Sukari – 1/4 kikombe au kulingana na ladha 🍬
Maziwa fresh au tui la nazi – 1 kikombe (sehemu ya kwanza) + zaidi kama uji utakuwa mzito 🥛
Iliki ya unga na vanilla – kiasi kwa harufu nzuri 🌿
📝 Jinsi ya Kuandaa:
1️⃣ Chemsha maji:
Weka maji kwenye sufuria, yaache yapate moto lakini yasifike kuchemka kabisa.
2️⃣ Ongeza mtama mzima:
Mimina mtama uliosafishwa. Acha uanze kuchemka kwa moto wa wastani.
3️⃣ Ongeza chumvi:
Weka chumvi kidogo sana kwa ladha ya mwanzo.
4️⃣ Pika mpaka mtama uive na maji yapungue:
Koroga mara kwa mara kuhakikisha uji hauwashiki chini ya sufuria. Mtama unatakiwa kuwa laini lakini bado uendelee kuwa na umbo lake.
5️⃣ Ongeza siagi:
Ukiona maji yamepungua na mtama unaiva, weka siagi koroga vizuri mpaka iyeyuke. Inaleta utamu wa kipekee.
6️⃣ Ongeza sukari:
Weka sukari kadiri upendavyo na uchanganye.
7️⃣ Ongeza MAZIWA (sehemu ya kwanza):
Weka kikombe cha kwanza cha maziwa au tui la nazi. Koroga vizuri mpaka maziwa yaingie vizuri kwenye uji.
8️⃣ Ongeza iliki na vanilla:
Weka kiasi kidogo cha iliki ya unga na vanilla kwa harufu nzuri na ladha ya kupendeza.
9️⃣ Pika na kagua uzito wa uji:
Endelea kupika na ukiona uji ni mzito sana, ongeza maziwa tena kidogo kidogo mpaka ufikie uzito unaopenda. Uji wa mtama haupaswi kuwa mzito sana bali uwe na hali ya kuenea vizuri kwenye kijiko.
🔟 Malizia kwa kupika taratibu:
Acha uchemke vizuri kwa dakika 5–10 kwa moto mdogo. Kisha zima jiko, koroga mara ya mwisho na upakue kwenye bakuli.
📝 Vidokezo vya ziada:
Kama hutaki kutumia maziwa ya ng'ombe, tui la nazi linafanya kazi nzuri sana.
Uji huu unaweza kuunganishwa na vitafunwa vya asubuhi kama mkate wa ngano, maandazi au visheti.
Pia unaweza kutumia asali badala ya sukari kwa afya zaidi. 🍯
Maoni