Cheese crep

MAHITAJI YA CREPE (Kuta za nje).
Yai 1

Unga wa ngano – 1 kikombe

Maziwa – 1 kikombe

Chumvi kidogo

Mafuta kwa kupaka kwenye kikaangio
VIUNGO VYA KUJAZA NDANI (chaguo lako):

Mozzarella cheese au cheddar cheese (ya kukatika vipande au kusagwa)

Samaki wa makopo (kama tuna), nyama ya kusaga, au mboga mbichi kama spinach zilizokaangwa

Pilipili hoho, kitunguu na viungo vingine

VIUNGO VYA KUFUNIKIA (Coating).

Mayai mawili (kupigwa vizuri)

Mkate wa kusaga (bread crumbs)
πŸ₯£ MAELEKEZO:

1. Tengeneza crepe.
Changanya yai, unga, maziwa na chumvi kwenye bakuli. Piga hadi iwe mchanganyiko laini.
Weka kijiko kimoja cha mchanganyiko kwenye kikaangio chenye mafuta kidogo na kaanga kwa moto wa kati hadi iwe nyembamba kama chapati laini. Rudia hadi umalize mchanganyiko.
2. Jaza ndani ya crepe.
Weka kipande cha jibini au mchanganyiko wako wa ndani katikati ya kila crepe.
Kunja kama bahasha au roll.
3. Funika kwa coating:
Paka kila roll kwenye yai lililopigwa, kisha pitisha kwenye mkate wa kusaga hadi ifunikike vizuri.
4. Kaanga hadi iwe golden brown:
Weka mafuta ya kutosha kwenye kikaangio.
Kaanga kila roll kwa moto wa kati hadi iwe na rangi ya dhahabu (golden brown) pande zote.

Maoni