๐ Mahitaji:
๐ฅฃ Unga wa ngano – nusu kilo
๐งด Hamira – kijiko 1 kikubwa
๐ฅ Maziwa – nusu lita (yawe ya uvuguvugu)
๐ฌ Sukari – vijiko 3 vya chakula (zaidi kwa kujazia)
๐ฐ Mdalasini ya unga (cinnamon powder) – kiasi cha kupaka
๐ง Chumvi – robo kijiko cha chai
๐ง Margarine – vijiko 3 vya chakula (zaidi kwa kupaka juu)
๐ฉ๐ฝ๐ณ Maandalizi:
1. Tayarisha Hamira:
๐ฅ Changanya maziwa kidogo ya uvuguvugu na hamira kwenye kikombe. Acha ifure kwa dakika 5.
2. Changanya Unga:
Weka unga kwenye bakuli kubwa. Ongeza sukari ๐ง, chumvi ๐ง, na margarine vijiko 3. Changanya vizuri kwa mkono au kijiko.
3. Ongeza Hamira:
Mimina mchanganyiko wa hamira kwenye unga. Endelea kuchanganya huku ukiongeza maziwa ya uvuguvugu taratibu.
4. Kanda Mchanganyiko:
Kanda unga mpaka uwe laini kiasi – usiwe mgumu sana wala mlaini kupita kiasi.
๐ Acha uumuke (ukae hadi uvimbe mara mbili ya kiasi cha awali).
5. Tengeneza Rolls:
Kata madonge makubwa, kisha sukuma kama chapati – lakini iwe pana na sio nyembamba sana.
6. Paka na Roll:
Paka margarine juu ya donge lililosukumwa ๐ง, nyunyiza sukari ๐ฌ na mdalasini ya unga ๐ฐ.
Kisha roll (kunja kama chapati) mpaka mwisho.
7. Kata na Panga:
Tumia kisu kukata vipande, kisha panga kwenye trey au sufuria kwa kuoka.
๐ถ Topping:
Baada ya rolls kuiva, mimina maziwa ya sona ๐ฅ au homemade condensed milk juu yake kwa ladha ya kipekee. ๐
Tip: Unaweza kuzila zikiwa moto au baridi – zote ladha yake ni ya kupendeza sana! ๐ง❤️
Maoni