JINSI YAKUPIKA TRIANGLE


Mahitaji

Nyama ya kusaga (kiasi unachotaka)

Viungo vya nyama ya kusaga:

Kitunguu saumu (thomu)

Tangawizi

Pilipili manga

Mdalasini ya unga

Karafuu ya unga

Chumvi

Maganda ya limao au limao

Pilipili ya kusaga (optional)


Mayai 3

Karoti 1 (iliyokatwakatwa au kupgrated)

Kitunguu maji 1-2

Pilipili hoho (pili pili boga)

Curry powder

Piki m powder (au garam masala)

Pilipili ya kusaga (ya kuwasha)

Baking paper

Mafuta ya kukaanga

Maelekezo:

1. Pika Nyama ya Kusaga

Weka nyama ya kusaga kwenye sufuria.

Ongeza viungo vyote vya kusaga nyama (kitunguu saumu, tangawizi, pilipili manga, mdalasini, karafuu, chumvi, nk).

Usiongeze maji. Pika hadi nyama iive na ikauke maji yake ya asili.


2. Andaa Mchanganyiko

Katika blender, weka:

Mayai 3

Nyama uliyopika

Karoti

Kitunguu maji

Pilipili hoho


Saga hadi mchanganyiko uwe laini kabisa.


3. Ongeza Viungo vya Ladha

Mimina mchanganyiko kwenye bakuli.

Ongeza curry powder, piki m powder, na pilipili ya kusaga (ya kuwasha).

Koroga vizuri hadi kila kitu kichanganyike sawasawa.


4. Oka Mchanganyiko

Washa oveni yako kwa nyuzijoto 180°C.

Tandika baking paper kwenye treya ya kuokea.

Mimina mchanganyiko juu ya baking paper kwa usawa.

Oka hadi mchanganyiko uwe umeiva na umekauka vizuri (kama mkate wa nyama).


5. Kata Triangle

Baada ya kuiva, toa kutoka kwenye oven.

Acha ipoe kidogo kisha kata umbo la pembetatu (triangle).


6. Kaanga Triangle

Piga yai kwenye bakuli.

Chovya kila triangle kwenye mayai yaliyopigwa.

Kaanga kwenye mafuta ya moto hadi ziwe golden brown.


Tayari Kula!

Unaweza kula triangle hizi na chai, juisi au hata kachumbari kama kando

Maoni