πŸ₯₯🍬 JINSI YA KUPIKA KASHATA ZA NAZI 🍬πŸ₯₯


πŸ›’ MAHITAJI:

✅ πŸ₯₯ Nazi zilizokunwa – vikombe 5

✅ 🍚 Sukari – vikombe 6

✅ πŸ₯› Maziwa ya unga – kikombe 1

✅ 🍫 Unga wa kakao – kijiko 1 na nusu

✅ 🌸 Rangi ya pinki – kijiko 1 cha chai

✅ πŸ“ Harufu ya strawberry – kijiko 1 cha chai

✅ πŸ’§ Maji – kikombe 1 na nusu

πŸ‘©‍🍳 JINSI YA KUANDAA:

1. πŸ”₯ Chemsha sukari: Weka sukari na maji kwenye sufuria nzito, chemsha hadi sukari iyeyuke.


2. πŸ₯₯ Ongeza nazi: Tia nazi na songa bila kuacha hadi maji yakauke kabisa na mchanganyiko uanze kushikana. Punguza moto.


3. πŸ₯› Mimina maziwa: Ongeza maziwa ya unga, songa hadi mchanganyiko uwe mzito kama donge.


4. 🍫🌸 Gawa sehemu tatu:

Sehemu 1: weka kakao.

Sehemu 2: weka rangi ya pinki + harufu ya strawberry.

Sehemu 3: acha iwe ya asili (nyeupe).



5. πŸ–️ Sukuma kwa ustadi:

Paka mafuta mezani.

Tandaza na sukuma mchanganyiko wa kakao.

Juu yake tandaza wa pinki, sukuma.

Mwisho tandaza wa rangi ya kawaida.



6. πŸ”ͺ Kata vipande: Sukuma vizuri, acha ipoe kisha kata vipande upendavyo.


7. ❄️ Acha zipoe kabisa kabla ya kuhifadhi.

Maoni