BADIA ZA MUHOGO

MAHITAJI

Muhogo mbichi – vipande 5 (paruzwa)

Kitunguu maji – 1 kidogo (kimekatwakatwa)

Kitunguu saumu na tangawizi – kijiko 1 (kilichosagwa au kupondwa)

Binzari ya pilau (cumin) – kijiko 1 cha chai

Pilipili ya unga – kiasi (hiari)

Chumvi – kiasi

Mafuta – kwa ajili ya kukaanga


HATUA ZA KUPIKA BADIA ZA MUHOGO.

🍠Paruza Muhogo

Menya muhogo na uoshe vizuri.

Paruza muhogo kwa kutumia kibeu (grater).

Kamua muhogo ulioparuzwa kwa kutumia kitambaa safi au mikono ili kuondoa maji yake ya asili (ya sumu kidogo).

🍠 Changanya na Viungo
Katika bakuli, changanya muhogo uliokamuliwa na:

Kitunguu kilichokatwakatwa

Tangawizi na kitunguu saumu vilivyosagwa

Chumvi

Binzari ya pilau

Pilipili ya unga kama unataka iwe na ukali

🍠Tengeneza Mduara
Chota kiasi kidogo cha mchanganyiko kisha sukuma kwa mikono hadi upate umbo la duara au oval.
Hakikisha zimeshikana vizuri ili zisianguke wakati wa kukaanga.
🍠Kaanga
Weka mafuta ya kutosha kwenye sufuria na uyaache yapate moto wa wastani.

Kaanga badia hadi zibadilike rangi ziwe za kahawia ya dhahabu (golden brown) na ziwe crispy nje.

Zitoe na ziweke juu ya karatasi ya kuzuia mafuta 

VYA KUZINGATIA 
Muhogo haupaswi kuwa na maji mengi, ndio maana unakamuliwa – hii husaidia badia kushikana vizuri na kuiva vizuri.

Usikaange kwa moto mkali sana – zitachomeka haraka bila kuiva vizuri ndani.

Zitumie zikiwa moto, zinaenda vizuri na kachumbari au chai ya rangi

Maoni