Mahitaji vya katai (Sugee Cookies) 🍪✨
Unga wa ngano – kikombe 1½ 🥣
Sukari ya unga (icing sugar) – kikombe ½ 🍚
Vanilla essence – kijiko 1 cha chai 🌸
Mafuta ya kupikia (vegetable oil) – kiasi cha kutosha kufanya donge 🛢️
Hatua kwa Hatua:
1. Changanya viambato vikavu
Katika bakuli kubwa, tia unga wa ngano na sukari ya unga kisha koroga vizuri hadi vichanganyike. 🥄
2. Ongeza vanilla
Mimina vanilla essence kwenye mchanganyiko na uendelee kuchanganya. 🌼
3. Tengeneza donge
Anza kuongeza mafuta kidogo kidogo huku ukichanganya kwa mikono au kijiko kikubwa. Endelea hadi upate donge laini linalojishikilia vizuri – lisiloshikana sana wala kuwa na mafuta kupita kiasi. 🤲
4. Tengeneza umbo la biscuits
Chota kiasi kidogo cha donge, kisha tengeneza mipira midogo kwa kuviringisha mikononi. Tengeneza rounds ndogo ndogo. ⚪
5. Panga kwenye tray
Panga katai zako kwenye tray ya kuokea iliyowekwa karatasi ya kuokea au kupakwa mafuta kiasi. Weka nafasi kati ya kila moja. 📋
6. Bake
Oka katika oveni iliyopashwa moto kwa nyuzi joto 160°C kwa dakika 15–20, au hadi karai zianze kubadilika rangi kidogo (creamy golden). 🔥⏳
7. Zipoe
Toa kwenye oveni na ziachwe zipowe kabisa kabla ya kuzihamisha au kuzihifadhi. Zikiwa moto huwa laini sana na rahisi kuvunjika. ❄️
Maoni