🌸VILEJA VYA TENDE🌼

 🌸NAMNA YA KUPIKA VILEJA VYA TENDE🌼




MAHITAJI NA VIPIMO

🧈 Siagi - Robo kg

🍬 Sukari - Robo kg

🥚 Mayai - 4

🥥 Nazi ya unga - Nusu kikombe

🌽 Cornflour - Kikombe 1

🍦 Arki (essence) Vanilla - 1 tbsp

🎂 Baking powder - 1 tbsp

🥛 Maziwa ya unga - Nusu kikombe (sio lazima)

🍞 Unga wa ngano - Nusu kg

🌴 Tende ya kusonga - Robo kg

🌾 Ufuta - Kikombe 1 (sio lazima sana)

🍮 Custard powder - Nusu kopo / 7-10 tbsp


NAMNA YA KUPIKA

Namna ya Kutayarisha na Kupika Vileja vya Tende

1️⃣ Saga Sukari na Siagi 🧈🍬 mpaka visagike vizuri.
2️⃣ Tia 🥚 mayai mawili mazima na mawili viini tu (ute weka kando).
3️⃣ Endelea kusaga, kisha tia 🍦 arki na 🎂 baking powder, saga kidogo.
4️⃣ Tia 🌽 cornflour, 🍮 custard powder, 🥥 nazi ya unga, na 🥛 maziwa ya unga, endelea kusaga mpaka kila kitu kichanganyike vizuri.
5️⃣ Anza kutia 🍞 unga wa ngano kidogo kidogo huku unachanganya kwa mkono mpaka linakuwa donge gumu kiasi – lisiwe gumu sana wala laini sana linashikamana vizuri mkononi.
6️⃣ Gawa madonge 5 hadi 6.

🌴 Kwa Tende:

  • Saga au toa kokwa za tende, kisha tia kwenye sufuria na 🧈 samli 1 tbsp.
  • Ipike kwa moto wa wastani ukisonga kama ugali mpaka inalainika.
  • Tia 🌾 ufuta, endelea kusonga kwa dakika 2-3, epua na wacha ipoe.

🍞 Kutengeneza Vileja:
1️⃣ Sukuma donge la unga mpaka liwe kama chapati.
2️⃣ Chukua 🌴 tende ulioisonga, iviringishe/isokote kwa mkono iwe nyembamba na refu, kisha isukume kidogo iwe flat.
3️⃣ Weka tende mwanzo wa unga uliousukuma, kunja pamoja na unga huku tende imo ndani mpaka ufike nusu ya ile round.
4️⃣ Chukua kisu, kata – sehemu iliyo na tende isokote tena na ikate kama visheti.
5️⃣ Panga kwenye trey au sufuria, paka ute wa 🥚 yai juu yake.
6️⃣ Ile nusu round iliyobaki, isokotee tena tende, na ufuate hatua kama mwanzo.

🔥 Kupika:

  • Bake kwa moto wa wastani mpaka vipige rangi ya light brown.
  • Ukivigusa vitakuwa laini, lakini vikipoa vinakazana na kuwa bora zaidi.

🎉 Enjoy! 😋
Vileja hivi ni vitamu mno kwa chai ☕ au kahawa ☕ na vina ladha laini isiyoelezeka!

Note: Ukihitaji idadi kubwa, ongeza vipimo mara mbili! 🥰

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUPIKA MIKATE YA CHILA (VIBIBI)

🌿🥩🍌NDIZI ZA NYAMA

VILEJA VYA JICHO LA NGAMIA

🥩🥗🍛BIRIANI YA NYAMA YA NG'OMBE

🍗🥘🍲PILAU YA KUKU

JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🍲

🍪🍯VILEJA VYA CARAMEL

JINSI YA KUPIKA VITUMBUA

🌼🌺VILEJA VYA JAM