👉VILEJA VYA CONFLAKES😉😍
RECIPE YA VILEJA VYA CORNFLAKES
MAHITAJI
Siagi 🧈: robo
Samli 🧈: robo
Sukari 🍬: nusu (kikombe au kiasi unachotaka)
Unga wa ngano 🌾: kilo kasrobo
Arki 🌸: kiasi (kwa ladha unayopendelea)
Baking powder 🧂: kijiko 1 cha chai
Mayai 🥚: 4
Cornflakes 🌽: kiasi .
NAMNA YA KUPIKA
🧈 Changanya siagi, samli, sukari, mayai 🥚, na arki 🌸.
🌀 Saga mchanganyiko wako kama unavyosaga keki hadi upate mchanganyiko laini.
🍚 Pembeni, changanya unga na baking powder 🧂.
🤲 Changanya mchanganyiko wa unga na siagi kwa mkono hadi uchanganyike vizuri.
Tengeneza viduara vidogo vidogo. ( au ✂ Kata kwa design unayopenda, kwa kutumia vikata au umbo lolote.)
Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni.
🔥 Choma kwenye oveni 🕐 hadi vileja vianze kupiga wekundu kidogo lakini visichomeke sana. viwache viwe na rangi ya vyeupe vyeupe.
💬
Maoni