🌼🌺VILEJA VYA JAM
VILEJA VYA JAM NA LOZI
VIPIMO:
- Unga – 2 Vikombe 🍞
- Sukari ya icing – 1 Kikombe 🍰
- Siagi – 250 gm 🧈
- Yai – 1 🥚
- Vanilla – 2 Vijiko vya chai 🍦
- Baking powder – 1 Kijiko cha chai 🥄
- Jam – ¼ kikombe 🍓
- Lozi – ¼ kikombe 🌰
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
- Koroga siagi 🧈 na sukari 🍚 katika mashine ya keki 🎂 mpaka iwe laini (creamy).
- Tia yai 🥚 na vanilla 🍦, koroga mpaka mchanganyiko uwe laini kama sufi.
- Tia unga 🍞 na baking powder 🥄, changanya na mwiko.
- Chota mchanganyiko kwa mkono (kiasi cha kijiko kimoja cha supu 🍲, fanya duara, kisha weka kwenye treya ya kupikia 🍽️.
- Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole 👆, kisha weka jam 🍓 na tupia lozi 🌰 zilizomenywa na kukatwa katwa.
- Pika (bake) katika oven 🔥 moto wa 375°F kwa muda wa dakika 15 hivi, huku unazitazama.
Maoni