🥮🍪VILEJA VYA CHOCKLATE
VILEJA VYA CHOCKLATE NA NJUGU
MAHITAJI
🍞 Unga - 300gm
🧈 Siagi - 225gm
🍭 Icing Sugar - 60gm
🍫 Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate) - 225gm
🍦 Vanilla - Vijiko 2 vya chai
🥚 Yai - 1
🎂 Baking Powder - ½ kijiko cha chai
🥜 Njugu za vipande - ½ kikombe cha chai
🥜 Njugu zilizosagwa - ¼ kikombe cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1️⃣ 🧈 Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini.
2️⃣ 🥚 Mimina yai na 🍦 vanilla, kisha koroga vizuri.
3️⃣ Mwisho, mimina 🍞 unga na 🎂 baking powder polepole mpaka ichanganyike vizuri.
4️⃣ Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda, kama ⭐ nyota, 🔺 pembetatu, ⚫ duara, au ❤️ kopa.
5️⃣ Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350°C. Vikibadilika rangi kidogo tu, vitoe.
6️⃣ Yayusha 🍫 chokoleti, kisha tia kwenye bakuli ndogo.
7️⃣ Paka kwa kijiko au chovyea upande mmoja wa biskuti kwenye chokoleti.
8️⃣ Nyunyizia 🥜 njugu za kipande na 🥜 njugu ya unga juu ya biskuti.
9️⃣ Panga kwenye sahani – tayari kufurahia na ☕ chai ya maziwa au kahawa!
Maoni