🥮Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa
Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa (Cocoa Coffee Biscuits)
MAHITAJI
💧 Maji baridi – Kikombe 1
🍪 Biskuti za kawaida – Paketi 2
🍫 Kaukau (cocoa) – Vijiko 3 vya kulia
☕ Kahawa ya unga – Kijiko 1 cha kulia
🥜 Njugu mchanganyiko zilokatwakatwa – Kikombe 1
🍬 Sukari – Kiasi upendavyo
Namna Ya Kutayarisha na Kupika
1️⃣ Changanya 💧 maji na 🍫 kaukau, ☕ kofi, na 🍬 sukari vizuri.
2️⃣ Katakata 🍪 biskuti kisha tia paketi moja na nusu ya biskuti kwenye mchanganyiko, achanganye vizuri.
3️⃣ Kisha nusu ya biskuti zilobakia, katakata vipande vikubwa na weka juu ya mchanganyiko, changanya kidogo tu.
4️⃣ Weka kwenye foil paper na zungusha (roll).
5️⃣ Fungua na umwagie 🥜 njugu au mkassaraat zilizosagwa juu.
6️⃣ Roll tena kwenye foil paper na uweke kwenye freezer mpaka igande.
7️⃣ Kisha kata kata slices na iko tayari kwa kuliwa! 😋
Maoni