NAMNA YA KUPIKA BIRIANI YA NYAMA YA NG'OMBE VIPIMO VYA MASALA Nyama vipande: 3 LB 🥩 Mtindi: ½ kopo 🥄 Kitunguu (thomu/galic): 1½ kijiko cha supu 🧄 Tangawizi: 1½ kijiko cha supu 🌿 Nyanya: 2 🍅 Pilipili mbichi: kiasi 🌶️ Nyanya kopo: 4 vijiko vya supu 🍅 Vidonge supu: 2 💊 Pilipili nyekundu paprika: kiasi 🌶️ Bizari zote saga: 2 vijiko vya supu 🌿 Viazi: 4 🥔 Mafuta: 2 mug 🛢️ Samli: ½ kikombe 🧈 Vitungu: 6 🧅 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kwenye sufuria, tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, na tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi, kisha changanya vyote pamoja na weka motoni. Katika sufuria nyingine, tia mafuta na samli, kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi, kisha toa na weka pembeni. Kanga viazi na weka pembeni. Chukua mafuta kidogo uliyokangia, tia kwenye nyama, acha kwenye moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke. Tia viazi na vitunguu vivunje-vunje, tia ndani ya nyama, acha ...
Maoni