🍮 HALUWA(HALWA)
🍮 JINSI YA KUPIKA HALUWA(HALWA)
MAHITAJI
💧 Vikombe 3 vya maji
🍬 Vikombe 4 vya sukari ya brown
🌼 Bana kidogo ya zafarani iliyochanganywa na vijiko 2 vya maji ya waridi (rose water)
🎨 Bana kidogo ya rangi ya machungwa na nyekundu
🔥 Maji yanapokaribia kuchemka, ongeza:
🥄 Kijiko 1 cha chai cha nutmeg ya unga
🥄 Kijiko 1 na nusu cha chai cha hiliki ya unga
🥣 Vikombe 2 vya unga wa tapioca/cornflour
kwa kuchanganyia unga
💧 Kikombe 1 cha maji
NAMNA YA KUPIKA HALUA
Roweka majani ya chai vikombe 2 vya maji ya moto upate rangi iliyokoza.
Chuja kwenye sufuria kubwa, mimina maji lita tatu na nusu au birika ya umeme mawili ya maji.
Kwenye hayo maji tia sukari, iliki, maji ya majani ya chai, zafarani na arki. Wacha mpaka ichemke.
Wakati sufuria ipo jikoni, chukua kibakuli, utie unga wa cornflour na uchanganye na vikombe viwili vya maji ya kawaida.
Mchanganyiko ukishaanza kuchemka, mimina ule unga uliouchanganya na maji. Koroga bila kuachia mkono kwa kutumia mwiko mrefu.
Ukiona mchanganyiko umeshashikana sawa sawa, mimina samli vikombe viwili.
Endelea kukoroga bila kuachia. Mchanganyiko ukiwa mzito, ongeza samli na endelea kukoroga.
Muda wote koroga kwa mzunguko wa kuelekea upande mmoja tu (clockwise au anticlockwise).
Koroga kwa masaa mawili hadi mafuta yajitenge na halua, na mchanganyiko uanze kuruka ruka.
Ili kujua kama halua imeiva, chota kwenye kijiko kidogo na uiache ipoe. Ikiwa ngumu baada ya kupoa, halua iko tayari. Ikiwa laini sana, endelea kupika huku unaendelea kukoroga.
Ikiwa tayari, tenganisha mafuta yote na halua.
Mimina halua kwenye trays au vibakuli vya kufunika na upambe kwa lozi zilizokatwa katwa.
Maoni