JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🍲
.jpg)
JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🍲 MAHITAJI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🥘 Njegere – Nusu kilo Nazi – 2 Nyanya – 4 Karoti – 1 Pilipili hoho – 1 Kitunguu maji – 1 Thoum – Kiasi Mafuta ya kupikia – Kiasi Chumvi – Kiasi JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI 🍲 Chambua njegere , zikoshe, kisha zitie kwenye sufuria na maji uzichemshe ziive kiasi, lakini zisilainike sana. Safisha nyanya , uzimenye na kuzikata. Pia katakata hoho , karoti , na vitunguu . Twanga thoum . Kisha, chujia tui la nazi zito na jepesi. Bandika sufuria jikoni, weka mafuta ukaange vitunguu , vikishabadilika rangi tia hoho , kaanga kidogo kisha utie thoum , nyanya , pamoja na karoti , endelea kukaanga. Mimina njegere , tia chumvi na mimina tui la nazi jepesi , wacha lichemke. Kisha tia tui la nazi zito liache lichemke kiasi mpaka uzito wa njegere ...