Mikate ya Ufuta Recipe π
Mikate ya Ufuta Recipe π
Mahitaji:
Vikombe 3 vya unga π
Vijiko 2 vya chai ya yeast π
Vikombe 2 1/2 vya tuwi la nazi π₯₯
Nusu kikombe cha mbegu za ufuta π°
Vijiko 2 vya yogurt (hiari) πΆ
Nusu kijiko cha #Sunsalt (chumvi) π§
Yai 1 (la ukubwa wa kati) π₯
Siagi au margarine kwa kupaka π§
Kwenye kupika mikate ya ufuta ni vizuri kuwa na pan kuanzia mbili, hii itakupa urahisi wa kupika pishi hili.
Namna ya Kutayarisha:
1. Changanya unga na chumvi, yai, na yeast. Ongeza tuwi la nazi na yogurt kisha koroga mpaka mchanganyiko uwe wa kuvuta (utakuwa na texture ya mvuto).
2. Funika mchanganyiko na uache upandishe mpaka ukubwa wake uongezeke mara mbili. Ikiwa unataka ladha ya kipekee, unaweza kuacha inavyoongezeka mara mbili.
3. pasha pan ya kupikia kwa moto wa kati, kisha nyunyiza maji ya chumvi na mimina mchanganyiko kiasi juu yake. Tumia mikono yako kusambaza mchanganyiko kwa unene wa nusu inchi.
4. Nyunyiza mbegu za ufuta juu ya mchanganyiko na acha kwa dakika 3 hadi 4.
5. Geuza mkate kwa kugeuza pan na uendelee kuupika upande mwingine mpaka uwe rangi ya kahawia ya dhahabu. Hakikisha usiuchome.
6. Epua pan ukion tayar mkate umeshaiva vizuri, ipoze pan yako Ondoa mikate kwenye pan na paka siagi juu yake.
7. Tumia pan nyengine na kuendelea na mikate yako hadi utakapo maliza, ni vizuri kuwa na pan mbili za kupikia ili upike kwa haraka.
Maoni